Sunday, May 27

Mmeshafanya homework?


Kama kawaida...Bibi to the rescue! (what will I do without you mama?) Namba 3 ilinishinda mie, afu nna hasira za karibu, ikabidi bibi achukue usukani, waende taratibu hadi kieleweke!
Kwa wale wenye schoolers wawe wa vidudu, primary au sekondari nawakumbusha tu kufanya homework, kama ulisahau...
Lunch itakua ishaliwa, mdau ameshashiba, kama ilisahaulika, basi homework ifanyike, ili kesho asitoe hadithi ya mbuzi kala daftari langu kwa ticha!

Hizi homework si za watoto tu, na wazazi tunahusika...fanya naye, hata kama wa sekondari jihusishe kwenye anoyojifunza, ili ujue ana uelewa gani...hata kama una elimu ndogo kuliko yeye, ukisoma hapa basi si unajua kusoma, basi soma naye somo la Kiswahili, ukiwa artistic kama kina mie, basi msaidie hata kupaka rangi...

Sio unamwachia anko, anti, sometimes dada kila siku...au mama kumwachia baba, or baba kumwachia mama kila siku--hafai. Afu akipata zero unashangaa, sasa kama ulikua hufatilii unaishia kujisifu tu "mwanangu ana akili, anajua bilinganya kwa kizungu, yaani full english, kiswahili hata hajui!" utajuaje            kuwa anaelekea kwenye zero???

Swali ni mmeshafanya homework leo? Kama bado FANYA sasa!



2 comments:

health baby happy baby said...

hi mama na mwana blog, i like the angle you cover; very educative. Keep informing and challenging us.

Jiang said...

Thanks for your support...Karibu tena.