Monday, May 28

Malaria haitibiki- dawa FEKI!


Nani hajaumwa malaria? Nani malaika wake hajaugua malaria?
Ukiumwa kichwa kitu cha kwanza kuhisi ni malaria, sometimes hamna hata kwenda hospitali, unajinywea dawa mseto, unakua poa.



Utajisikiaje ukijua kuwa zaidi ya asilimia 20 ya hizo dawa ni FEKI!!??
Si dawa si chochote thus hazitibu malaria.

bonyeza hapo kushoto (palipoandikwa zaidi bofya hapa) kwa taarifa zaidi...


Unadhani malaria ni ugonjwa wa kuchezea? Unaua kuliko Ukimwi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kwamba WATOTO 2,000 wanakufa KILA SIKU barani Afrika kutokana na malaria...bado unadhani ni ugonjwa mdogo?

Utafiti uliofanywa karibuni ndio umeonyesha ufeki wa madawa hayo tunayoyaamini kulinda afya zetu!
Utafiti huo umeonyesha kuwa kwenye nchi 21 za Sub-Sahara, asilimia 20 ya zaidi ya dawa 2,500 zilizofanyiwa majaribio zilikua FEKI, huku asilimia 35 hazikutimiza viwango!

Kwa hili mie nimenyoosha mikono juu, maana sijui la kufanya, hata serikali yetu haihusiki hapa, ila TBS inaweza kutusaidia (???) mmmh!!! otherwise tubaki tunalia tu na malaria zetu!


Story nzima longa na Al Jazeera

No comments: