Monday, May 14

Umenyonyesha muda gani? Are you a mom enough?

Hii nni cover ya time iliyoleta utata sana huko kwa wenzetu...
Kwanza ni hiyo headline ya Are you a mom enough?
na kwa wenzetu huko ambako kunyonyesha hadharani ni issue ya kuweka picha ya mtoto anayonya kama hivi pia ni balaa.
Ila kubwa zaidi ya yyote ni kwamba watoto waachishe kunyonya lini? 
Huyu mtoto anakaribia miaka minne.

Nimenyonyesha watoto wangu, wa kwanza miezi sita na wa pili miezi saba tu, am I a less mom kuliko aliyenyonyesha mwaka mzima au miaka miwili?
Na asiyenyonyesha kabisa, je yeye ni less mom kuliko walionyonyesha? 
Mama, baba tupia comment yako hapo chini!

Article yenyewe kuhusu njadala wa hii issue hii HAPA!

9 comments:

Anonymous said...

nimenyonyesha miaka miwili, nadhani inatosha jamani khaaaa miaka minne hapana, pia mtoto atakuwa mjinga sana kama ukimnyonyesha hadi anajitambua

Anonymous said...

It depends with ur daily activities, kwa mujibu wa wataalamu wa afya ya mtoto, kiukweli anatakiwa anyonye miaka miwili na inasadikika watoto walionyonya muda mrefu wanakuwa na akili sana. Lakini kutokana na changamoto za maisha kunyonyesha mtoto hata kwa mwezi mmoja ni shughuli kwa wazazi wengi wa sasa. Kila mama ni kamili muda wa kunyonyesha si jambo muhimu kikubwa ni kujali afya ya mtoto. Ila kwa wale wanaotupa watoto hawamo kwenye kundi la kinamama walio kamili.

Unknown said...

DAH HUU UTATA AISEE. ME NADHANI KADRI UNAVYOWEZA ILA ISIZIDI SANA.HATA 6 MONTH IT'S OK AS LONG AS SIKU HIZI KUNA SUPPLEMENTS AMBAZO ZAMANI HAZIKUWEPO ,MIAKA MINNE SI NDIO YALEYALE YA KUJA KUAMBIWA MBELE ZA WATU WE MAMA EMBU KAA CHINI UTOE LINYONYO LAKO NINYONYE?

Anonymous said...

Wamama tumekuwa tunawasahau sana atoto wenyesababu ya kazi. Mtoto anatakiwa kunyonya kwa muda usiopungua miaka 2, hii inamjenga mtoto kiakili na hata kuimarisha kinga za mwili.Hata kama tunakuwa busy at least ule muda unaopata wa kukuaa nyumbani mtoto anyonye. Pia unaweza kukamua maziwa ukaweka kwa chupa yake, maziwa ya mama yanauwezo wa kukaa masaa 8 bila kuharibika yakiwa na joto lake lile lile ilimradi tu chupa ya mtoto iwe safi na iwe sterilized.

Anonymous said...

Kwa nutrition sake wanasema miezi 12 ndio sawa. Lakini hii ni spe kubwa sana ukizingatia miaka 10 iliyopita hata kusema kunyonyesha ilikua unaweza kuhukumiwa. Ilikua ni tusi kubwa sana.

Hiyo mom enough ni trend tu kwasababu vitu vyote hao wamama wanaojiitia hivyo wanavyovifanya sisi kwetu ni normal. Juzi hii cover ilivyotoka mimi nilikua nabishana nao..Ninafanya vyote hivi lakini sijiiti mom enough..Kwtu ni kawaida kwao sio kawaida ndio maana hiiissue imetokea.

Kwetu sisi tunalala na watoto chumbani kwao mtoto akitoka hozpital wa siku 3 analala mwenyewe chumbani kwake. Sasa wanao lala na watoto wao wanaona wao ni more than the other.

Sisi kwetu tunabeba watoto kwa mgongo wao ni kusukuma mtoto kwenye stroller toka amezaliwa. Sas siku hizi nao wameanza slings sasa mtu anayefanya hivyo basi anajiona yey eni more than the rest.

Sisi kwetu tunanyosha wao ilikua hawanyonyeshi kwabisa sasa toka wameanza kujifunza kunyonyesha basi ndio wengine wanajiona wao ni more than those who don't or can't...

Lakini yote hayo ni kuwa attached na watoto. Sisi tunafanya vitu vyetu natural wao ni kwa ajili ya trendy au doctor amemwambia afanye hivyo.

Mimi mtoto wangu 3yrs na 2 months now bado ananyonya..well nilianza kumwachisha akiwa na miezi 20. Nikatumia vidonge fulani wanasema vinafanya maziwa yasiwe matamu lakini hakuacha na mimi nilitumia siku 7 tu nikasema sitaki kunywa mavitu hata sijui ni nini niweke kwa mwili wangiu na mwanangu. Then nikatumia pilipili mpkaaa sasa hivi ananyonya akisema itch itch lakini haachi. Ila kwa vile mchana hatupo pamoja hivyo ni usiku tu. Nafikiria ataacha akipenda..mimi nilinyonya mpaka nina miaka 5 ila mama sasa hivi anasema wewe ulinyonya mpaka miaka 3 but I do remember..So kwa maoni yangu na doc amendiambia nutrition sasa hivi sio muhimu lakini study imeonyesha the longer wananyonya the smarter they get...

mama k said...

kama your kid is smart nothing can change that hata umyonyeshe miaka 7... i have a baby and nimemnyonyesha 8months and namlea vizur kwa mapenz yote, she is smart and she haz all thhe love i can give her as a mother...
so being a mom enough or not cannot be determined kwa how long umenyonyesha mwanao...ni malezi bora unayompa kiroho, kiakili na kimwili..

Mama J said...

Mjadala huu nimeufurahia sana. Sikuwahi kufikiria kwamba mtoto anaweza akanyonya hata akiwa na miaka minne! mmh! njino! Enewei, inawezekana ninashangaa kwasababu mie maziwa yangu ya kubangaiza. Mwanangu ana mwaka na miezi mitano tu lakini kifua almost kimekauka ingawa bado anavutavuta kidogo anachomudu kukikamua! Natamani sana kumnyonyesha hadi miaka miwili lakini kuna kila dalili kwamba siku si nyingi maziwa yatakata. Inawezekana wadau mnafahamu vyakula ambavyo vinamsaidia mwanamke kuproduce maziwa ya kutosha, nisaidieni maana kila ninachotajiwa nakisaka kama mwendawazimu!Nilitajiwa nyanya chungu nikazitafuna kama sina akili nzuri, nikatajiwa pipipili mtama nikawa naweka kwenye supu na hata katika chai mwisho nikaona nitatoboa utumbo! Nikatajiwa nanasi nikawa nakula nanasi zima mpaka nikachubuka mdomo! Nikatajiwa korosho nikawa nakula hadi najisikia vibaya, sanasana nimeongezeka uzito! Msaada tutani wadau!

Anonymous said...

mjadala mzuri, nammnyonyesha mwanangu mwezi wa nne sasa na natarajia kumuachisha baada ya miezi 9 kulingana na nature ya kazi yangu..nina maziwa mengi sana naturally situmii kitu chochote na mpaka sasa mwanangu ananyonya maziwa yangu tu..japo asubuhi napokuwa kazini mpaka saa 8 anatumia maziwa ya kopo yanaitwa sme jaman kuna madhara yoyote katika hilo?? naomba ushauri wenu wadau.

Anonymous said...

Yote mema tu wadau kama alivyosema mwenzetu hapo juu. Kinachomata mtoto anapata mapenzi ya mama na chakula chakutosha.

Mie wangu ana miezi 21 hata sijui lini ataacha maana mbishi kweli na akiniona tu nikunyonya kwanza ndo akacheze, usiku ndo usiseme halali hadi sasa chuchu ina kleki, nipo mbioni kumuachisha ila sielewi nitaanzia wapi? au nitamdanganyia nini ikiwa maziwa ya aina nyingine yote hataki tangu azaliwe.

Msaada wadau!