Wednesday, May 16

Usafi wa meno ya mtotoMtoto anapaswa kuanza kusafishwa meno pale tu baada ya kuota. 

Usiulize vijino viwili mswaki wa nini...mswaki lazima hata kwa kijino kimoja!

Wazazi wengi tunajisahau sana katika hili hivyo kuyafanya meno ya 
watoto wetu kuwa machafu na kukosa ung’aavu.


Mtoto anapaswa kupigishwa mswaki kwa kutumia dawa ya meno ya watoto.
  Dawa za watoto

Dawa za meno za watoto zipo nyingi sana na za aina mbalimbali. Tofauti ya dawa hizi na zile za watu wakubwa hizi hazina madhara hata kama mtoto ataimeza kwa kuwa haina fluoride.

Pia mswaki wa mtoto utumike ili kuepusha kumuumiza kwani umetengenezwa laini kulinganisha na ugumu wa fizi zake.Miswaki ya watoto 

Tembelea Supermarkets kujichagulia dawa ya meno na miswaki ya mwanao.

Kwa taarifa zaidi juu ya usafi wa meno ya mtoto ingia HAPA 

1 comment:

Anonymous said...

Sio lazima mpaka meno yaote; tunashauriwa kuanza kuwasafisha watoto kabla ya meno kutoka. Unaweza kumsafisha kwa kitambaa safi na maji ya vuguvugu. Na akisha fikia miezi 4 au 6 unaanza kumswaki na "training tooth brush" kwa wenzetu wa nje wanajua zaidi. Ila kama huna uwezo wa kununua miswaki ya kitoto unaweza tumia kitambaa.