Gud mamaz,
Kuna matukio mbalimbali yanayotokea mitaani kwetu ambayo ni unyanyasaji wa watoto. Lakini
labda huenda wanaoyafanya hawajui kama huo ni unyanyasaji.
Mamaz mnazungumziaje swala la mtoto kufanyiwa KINDUMBWENDUMBWE,
eti kwa kuwa amekojoa
Kitandani?
Kwa msiojua;
Kindumbwendumbwe:
Ni
kitendo cha kumzungusha mtoto mtaa mzima,
akiwa na nguo zake alizozikojolea,
na
mashuka yakiwemo huku watoto wengine (na watu wazima wakati mwingine)
wakimfata
kwa nyuma wakimzomea na kumwimbia.
"Kindumbwendumbwe! Chalia! Kikojozi
kakojoa! Na nguo kazitia moto”
Hii kitu ina madhara kwa mtoto na inaweza kumjengea mtoto kutokujiamini,
kukosa raha na saa nyingine inaweza
kumfanya mtoto kuwa mkatili.
Ukiwa kama mzazi unakichukuliaje kindumbwendumbwe?
1 comment:
kwa maoni yangu ni unyanyasaji wa mtoto, kuna watoto wanaowahi kuacha kujikojolea tena watoto wa kike wanaacha mapema kuliko wa kiume sasa ukimuhukumu mtoto kutokana na maumbile ambayo yako nje ya uwezo wake ni kumyanyasa
Post a Comment