Wednesday, May 19

Angel wings zinapatikana wapi?

 Kama sijakosea, mara ya kwanza kabisa tuliziona kwa mdau Turnesh Ally (jina la kihabesh, nalipeeenda ajabu)...

...then akaja mdau Dorice, yake ya baby pink!!!

...wengi wenu mtamkumbuka fashonista in the making, Iqrah wa SHAMIM, mabawa yalimetch na gauni! kumbukumbu zangu zinaniambia ma'mtu alisema alitumiwa zawadi ya hii nguo, pamoja na mabawa yake, toka Sauzi!

mwezi huu tumebarikiwa malaika wawili...huyu Risper yake ni tofauti sana na ya wenzake, kama yana manyoya flani, afu kama anaweza kupaa nayo kweli!

...na Glory ndio malaika aliyeshuka Jumamosi, yake mekundu!

*****
Kusema kweli, hakuna mtoto asiyependeza na mabawa, hata kama kavaa kigauni simple, mabawa yanafanya awe tofauti na waalikwa, unaweza kuongeza na crown juu ukipenda...si utani nikijaaliwa mtoto wa kike lazima avae mabawa birthday party mojawapo kabla ya miaka minne, maana mi nayapenda sana!

Mama Candy aka Neema Chalamila wa Arusha pia anayazimia sana mabawa haya, na yeye ana malaika wake anayekaribia kutimiza miaka miwili. Malaika huyo kabarikiwa kila kitu, ila kakosa mabawa.
Neema anauliza wadau hayo mabawa ya malaika yanapatikana wapi? 
Hata kama Dar atayafata tu, maana anataka malaika wake naye apendeze siku yake!

7 comments:

tweety said...

Clean hearts like Angels

Anonymous said...

kweli mama X nami nilipenda kujua hilo!!

thanx!!

Anonymous said...

mama x nami napenda mwanangu avae jamani tuulizie kwa wakina mama glory watoto zetu nao wapendeze

Jiang said...

nimeuliza nimeambiwa Shoprite ya Mlimani city, section ya watoto ziko kibao, kila rangi! ila bei sijaambiwa.

Jiang said...

Jackline aka Mama Glory anasema Shoprite zinauzwa 10,000/-.

Jiang said...

nimepita Toto Junction, duka liko maeneo ya posta ya zamani, pia zipo nyeupe, dizaini kama Risper, bei ni 9,000/-

Anonymous said...

thanx mama X.
much love mama abby