Wednesday, May 16

Kindumbwendumbwe...



Gud mamaz, 


Kuna matukio mbalimbali yanayotokea mitaani  kwetu ambayo ni unyanyasaji wa watoto. Lakini labda huenda wanaoyafanya hawajui kama huo ni unyanyasaji.  

 Mamaz mnazungumziaje swala la mtoto  kufanyiwa KINDUMBWENDUMBWE,
 eti kwa kuwa amekojoa Kitandani?



Kwa msiojua;
Kindumbwendumbwe
Ni kitendo cha kumzungusha mtoto mtaa mzima,
akiwa na nguo zake alizozikojolea, 
na mashuka yakiwemo huku watoto wengine (na watu wazima wakati mwingine) 
wakimfata kwa nyuma wakimzomea na kumwimbia.


        "Kindumbwendumbwe! Chalia! Kikojozi kakojoa! Na nguo kazitia moto”


Hii kitu ina madhara kwa mtoto na inaweza kumjengea mtoto kutokujiamini,
 kukosa raha na saa nyingine inaweza 
kumfanya mtoto kuwa mkatili.


Ukiwa kama mzazi unakichukuliaje kindumbwendumbwe? 




1 comment:

Anonymous said...

kwa maoni yangu ni unyanyasaji wa mtoto, kuna watoto wanaowahi kuacha kujikojolea tena watoto wa kike wanaacha mapema kuliko wa kiume sasa ukimuhukumu mtoto kutokana na maumbile ambayo yako nje ya uwezo wake ni kumyanyasa