Saturday, June 2

Umetengaje muda wa kukaa na mtoto wako?

 Siku hizi watoto wanafanyiwa sana harassment; madada wetu wa kazi, wajomba, mashangazi, walinzi, majirani, watu wanaokutana nao shule, yaani ni kutoka kwa mtu yeyote, anaweza akawa ndugu, jamaa, rafiki au stranger!
Tatizo ni nini?
(bofya hapo kushoto tujadili)



Tatizo kuwa wazazi tuko busy na kusaka mshiko tunakuja kugundua tatizo likiwa limeshakuwa kubwa au mambo yameshaharibika kabisa.

Tunashukuru mapinduzi ya sayansi na teknolojia nayo kwa sasa yamechangia kwa kiasi kikubwa katika malezi ya watoto kwani sometimes badala ya kukaa na sisi wazazi muda mrefu wanakaa na TV wakicheki katuni, wakicheza game au hata wakiangalia vitu vingine ambavyo wazazi hatuvijui na hata tungevijua tusingeweza kuwaruhusu kuangalia.

Nakumbuka enzi za utoto wetu hivi vitu havikuwepo kabisa. Tulikuwa tunacheza mdako, kombolela na michezo mingine mizuriiii ambayo watoto wa siku hizi ni wachache sana ambao wanaijua.
Hakuna mzazi ambaye hapendi kukaa na mwanaye wakacheza wakafurahi lakini ugumu wa maisha umekuwa kikwazo kwa kweli.
Je umetenga muda wa kuzungumza na kuwasikiliza watoto wako? Au ndo kumwachia dada na TV vikimkuza?
Kama ulikuwa hujui vitendo vingi vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto hufanyiwa zaidi na watu wao wa karibu kama majirani, uncle, dada wa kazi nk.
 Ni vizuri tuwatengee watoto wetu japo Jumapili basi kama sio siku nzima hata masaa machache ili kusikiliza shida za mtoto na kupiga stori mbili tatu ili ujue yaliyo chini ya kapeti.
Tuzinduke na kuamka ili tutetee maisha ya watoto wetu.

No comments: