Thursday, December 13

BABA WA MFANO

Baba wa Mfano leo uso kwa uso na Selemani Msindi aka Afande Sele, pia anajulikana kama Afande Sele The'King kama anavyojiita kwenye mtandao wa kijamii wa facebook.

Anasema,
"Leo nilijikuta nikiwekwa chini ya ulinzi wa nyumbani na huyu Princess mdogo ASANTESANAA, baada ya mama yake (ASHA) & dada yake princess TUNDAJEMA(TJ) kutoka kwenda dukani kufanya manunuzi ya mwisho ya mahitaji ya shule ya TJ, kwa kuwa anaripoti shuleni pale Kunduchi Girls Islamic high school, hivyo ilibidi nibebe majukumu haya makubwa na mageni "mashikolo maggeni".... kwa wakati fulani, big up kwa akina mama wote duniani kwa kutuzaa na kutulea, na zaidi katika umri mdogo kama huu.. hard work pays .. life goes on.

Asante Afande Sele kwa kuwapa heshima wamama wote duniani.
Mama na Mwana inakutakia Malezi Mema.

No comments: