Tuesday, February 26

Malaika huyu ameokotwa asubuhi hii!

Wakati wengine wanatafuta, mtoto huyu ameokotwa akiwa ametelwkezwa kichakani Kimara mitaa ya njia ya GIDE asubuhi hii... wasamaria waliskia kanalia kichakani kwa kung'atwa na manyenyere na wadudu ndio wakakiokoa...
Amepelekwa hospitali ya Mwananyamala, anaendelea vizuri...

Ushauri wa bure tu kwa akina dada: Kuna vituo vingi vya kulea watoto, makanisa na misikiti! Kama unaona huwezi kulea mtoto mpeleke pale, kuna watu kibao wanalia na kukesha wakiomba wapate mtoto japo mmoja, afu we unapata unamtupa kichakani aliwe na wadudu kama mzoga wa mbwa, wakati ni binadamu mwenye uhai...kama humtaki mpeleke kituo cha kulelea watoto, watamlea tu, sio kufanya ukatili kama huu!
--Jiang.

2 comments:

Anonymous said...

jamani ee mungu mtu unakaa na mimba miezi 9 unazaa kwa uchungu kisha unamtupa mtoto!!mungu atamlaani huyo dada,nimefurahi kusikia anaendelea vzr huyo mtoto mungu amkuze inshallah.

Anonymous said...

nimesikitika sana kama hutaki mtoto mbona njia ziko nyingi sana ni kufata tu ili usizae mpaka utakapokuwa tayari sio kubeba mimb amiezi tisa halafu uzae kwa uchungu kisha umtupe