Tuesday, January 13

Majina ya Watoto Top Ten

Mdau wetu Sophy ndiye pekee jina lake lipo kwenye top ten hiyo. Kwa haraka haraka wengine waliopo kwenye hiyo top 100 ni Josh, Evelyn na Jada.
***
Hii kwa watarajiwa woote, ambao bado hawajapata majina ya watoto wao.
unatafuta jina unique na mabalo hadi mwenyewe aweze kuliandika anakuwa ana miaka 18 kama Xchyler, au linalojulikana na kila mtu kama Salim, au toka kwa supa star kama Jada na Thierry?
Whatever name unalotafuta, jina inaweza likawa ni kitu pekee cha muhimu sana kwa mtoto na hakina bei.
Basi kuna website flan ya mambo ya watoto nnayopenda kuitembelea inaitwa babycenter, imetoa list ya majina 100 maarufu zaidi kwa mwaka 2008 huko majuu kama yalivyopigiwa kura na watu wa huko.
Hapa nakupa top ten:

La Kike / La Kiume
  1. Emma / Aiden

  2. Sophia / Jayden

  3. Madison /Ethan

  4. Isabella / Jacob

  5. Olivia/ Caden

  6. Ava/ Jackson

  7. Madeline / Noah

  8. Adson / Jack

  9. Hailey / Logan

  10. Lily / Matthew

5 comments:

Anonymous said...

Hayo ya majuu, ina maana tuachane na ya kwetu kama chausiku, Nchumali, asajile? Na wachina nao waachane na yao kim, xiao, mshikaki? Acheni utumwa wa kudai eti majina ya celebs au watoto wao huko US ndio top ten!

Anonymous said...

wewe mama xchyler, kwanza cross check maandiko yako mana unakosea kosea, be neat and carefull mana unaandikia dunia nzima, lazma uwe professional bwana. eti website ya mabo ya watoto , yani nimerudi mara 50, unapotosha, muombe hata mtu akusaidie ku cross check kabla hujapost kitu

pili andika basi kwa font nzuri, na maandishi yenye mvuto, mana blog yako ni ya maana sana sema iko iko tu, haina mvuto, hata mtu anaona hamna cha maana, au nifungue yangu nikupiku nini, mana inaonekana hauko serious. inakua ya kishamba bwana

Anonymous said...

sasa mama xchley narudi tena na comment ingine kwa leo, kwa kweli issue ya majina kwa mtazamo wangu ni kitu sensitive sana, kwa maana ingine ni kitu cha kuzingatia mno, sio kumpa mtoto jina kwa ushabiki.

hata mimi ni mama, na hua napenda kumpa mtoto jina kulingana na maana, kwa mfano bahati, pendo, nk, unaweza ita majina hayo hata kikwenu ukipenda kama litasound better, huo ni mfano tu.

sasa sio kumpa mtoto jina ambalo, hata kulitamka au kulindika mpaka anafika sekondary hawezi, au unampa jina akimtajia mtu lazma aulize mara mbili, au jina ambalo akienda shule wenzake wamtanie, au majina ya kishabiki eti rhihana, oprah, whitney yani majina ambayo hata ukimtajia mtu lazma amkumbuke yule mtu famous mwenye jina.

kwa mfano ukisema unaitwa oprah lazma mtu aseme ooh oprah winfrey, au ELvis mtu lazma aseme ooh elvis presley. Jua kwamba wenye majina kama hayo wanakiri kukereka na watu kuwafananisha hivo na wana wish kubadili majina yao.

so usimpe mwana tabu, be carefull. Kwanza majina ya kizungu mpaka wazungu wanakushangaa we mbogo jina la kijerumani la nini au la ki swedish??????????????????????

Anonymous said...

jiang????????

nakushauri uwashauri watu waangalie meaning za majina sio jina ni jina tu, kama xchyler hata sijui linatamkwaje mpaka sasa, naomba uniambie please..... sijui ni chaila, au zaila au ekschailer au ekchila.

unajua utasababisha mwalimua akiwa anasoma attandance list ya watoto darasani atamke jina la mwanao vibaya alafu wenzie wamcheke na kumtania.............. atalichukia oh hooooo! mana watoto kuna umri amabo ukitaniwa unakuchukulia serious kweli, pia inaweza kumharibia mtoto self confidence, mana kila siku mwalimu mpya akiingia lazma akosee jina, alafu wenzie wanamcheka alafu walimu wengine watamuuliza ' we ndo jina gani hili umepewa?' au akikosea kitu utaskia 'we ndo mana hata jina lako halieleki, hilo jina mana yake itakua mapepe mana hujatulia' anyway this like that, mtoto anaweza kuathirika ki saikologia mana ni jina ambalo bongo hatujui kutamka na mwanao yuko bongo

Anonymous said...

Habari wadau..
mimi ndo leo natembele hii blog, na nmeipenda sana cna hakika hii post n ya lini but imenivutia ! ANONYMOUS hapo juu wa kwanza kabisa, comment yako imenikumbusha far, ninae mpenz wangu cku moja 2metembelea marafiki zake yan shemeji zangu sasa. Baada ya wake zao kujifungua.. Tulikuta tayari wamepewa majina, shemeji wa kwanza mwanae anaitwa Praise, wa pili mwanae anaitwa Brighton, na wa 3 mwanae anaitwa Fay. Mwenzangu alishangaa sana na kuuliza hiv mmekosa majina ya kwe2 jamani kama vile akina Kibuyu,bahati,chausiku n.k..walicheka sana, akasema msicheke mnaweza ita watoto majina kumbe kule kwao ni famous kwa wamyamawao au kitu flan,afu nyie huku mnawapa watoto!2naua ukoo taratibu mpe mtoto jina la bibi yako,baba,mama au co!