Sunday, January 11

Mdahalo Unafungwa: Watoto Kuonja Pombe

Kwanza kabisa utafiti kidogo sana umefanywa kuhusu madhara ya pombe kwa watoto, kwa hiyo hata kupata data ni kazi sana.
Utafiti uliofanywa na jarida moja linaloitwa Alcoholism: Clinical & Experimental Research unaonyesha kuwa unywaji pombe kwa watoto wadogo huwa unaanzia nyumbani, kwa watoto kuoja kidogokidogo.

Research hiyo inaonyesha kwamba watoto wanaoonja mara nyingi kama sio zote wanaishi na watu wanaokunywa pombe, yani ni wazazi au walezi wao ambao ni wanywaji, kwa hiyo ni rahisi kupata pombe ya kuonja.

KUZUIA MTOTO ASINYWE KAMA MZAZI NI MYWAJI
Kama wewe mzazi ni mywaji, na unakunywa nyumbani, mtot lazima atauliza unakunywa nini na atakua na hamu ya kutaka kuonja inatest vipi.
Suluhisho sio kugomba na kumkaripia mtoto, ila mtulize na umwambie kwamba ni pombe ila tumbo lake haliwezi kusaga kwa sababu yeye ni mdogo, akikua ataonja.

Ila kumbuka kwamba research zinaonyesha kuwa watoto wanaonjea pombe nyumbani hawawi walevi wa kutupwa na wala hawafanyi maamuzi ya kipuuzi kutokana na influence ya pombe.

Ni vizuri akaonja akiwa nyumbani bila ushawishi wa watu asiowajua na hapo nyumbani ni controlled environment, yani hata ikimzidia kwa bahati mbaya hawezi kufanya chochote cha ajabu, just imagina ameonja akiwa na marafiki zake mtaani, watataka kuonyeshana ubabe wa nani anakunywa zaidi na kuishia kulewa sana na kufanya mambo ya ajabu.

Hapa zingatia umri wa mtoto, kwa mfano mtoto wa miaka 18 anaweza akaonja wine kidogo iliyochanganywa na juisi au maji. Akiwa nyumbani utajua wapi pa kumkataza, mfano, glass moja ya wine iliyochanganywa na juisi inamtosha.

Ila kitu cha muhimu kuliko vyote is teach y example. Kama wewe mama au baba unarudi umelewa chakari, utamfundisha nini mwanao kuhusu pombe? Weka mfano mzuri kwa mwanao kama unakunya kwa kunywa responsibly, kwa kunywa kwa wastani tu.

Pia kumbuka kwamba haishauriwi kabisa kwa mtoto mdogo kunywa pombe, hata kama ni kuonja tu.
***
Asanteni wote mliochangia mdahalo huu.
Kama kawaida, kesho, tunafungua mpya, stay tuned...

No comments: