Thursday, January 22

Uzi Mweusi Mkononi Kwa Mtoto

Huku mitaani kwetu, hasa ukwa sisi tunaoishi uswahilini ni kitu cha kawaida kabisa kuona mtoto amefungwa uzi mkononi, wenyewe wanasema unafukuza watu na vitu vibaya wanaotaka kumdhuru mtoto. Wadau hiyo imakaaje kaaje, na kwa waliowahi kufanya hivyo watupe faida zake, ukute utandawazi unatuharibu, vitu vingine vina faida tunadharau.

7 comments:

Anonymous said...

Hi Jiang,
Unajua imani inajenga, wale ambao imani yao inamtuma kumfunga mtoto kitambaa cheusi mkononi kwa kuamini ya kwamba anamzuia na mabaya pamoja na watu wabaya, basi kwa imani yake anaamini ni kweli. Lakini kama mtu hana imani hiyo ataweza kuamini kama kile kitambaa kitamkinga mtoto. Wale wenye imani hiyo watusaidie na kutuambia inaweza kusaidiaje hicho kitambaa?

Mama S

Anonymous said...

Bwana Jiang usisikie, kile kitambaa cheusi kinafanya kazi. Ndani ya kile kitambaa cheusi kuna dawa inaitwa mvuje, una harufu kali kidogo, ule mvuje ndio unasaidia kufukuza mambo mabaya yanaowafuata watoto wadogo. Na sizungumzie hirizi.

Baba Jackson

Anonymous said...

Habari zenu,mimi nadhani kama mila yako inakuruhusu mfanyie mwanao bwana,mbona kuna majani ya kumuogeshea mtoto

So tuache uzungu sana,let's do ambayo tulikuwa tunafanyiwa ila vyengine unakataa ambavyo kwa logic unaona mhhh hii hapana

Francis said...

mie naona huo ni UONGO MTUPU!!
toka lini kitambaa kikamlinda mtu??
tutumie hata common sense jamani.
by FML

Anonymous said...

hamna lolote, mambo ya kiswaz tu, mbona huku nje watoto hawafungwi na hamna mabaya yanayowapata? Mungu ndo mlinzi wetu pekee.

Anonymous said...

HAMAN LOLOTE, MWANANGU HAJAVAA ULE UZI BADO and no way atavaa, haina kinga yoyote uzushi tu

Anonymous said...

Ni suala la imani tu. Hakuna sababu ya kumvalisha, kila jambo lapangwa na Mungu.Kikubwa ni jukumu la wazazi, baba na mama kuwalea watoto kwa kuzingatia lishe bora na usafi maradhi hayatamsumbua, kama yatakuwapo ni ya kawaida na si kutokana na macho ya watu. Umwache mtoto ang'atwe mbu useme ni macho ya watu!