Thursday, May 21

Mbagala sio mabomu peke yake...


Wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Maendeleo huko Mbagala Kuu karibu na mabomu wakifanya mtihani wa moko jana. (Picha hisani ya BongoPicha)
*****
Kufanyia mtihani chini sio kwa ajili ya mabomu, ni tatizo la siku zote, walimu kwa kutumia akili zao (ambazo mimi zimenishangaza) waliamua wanafunzi hao wafanyie mtihani huo wa moko chini kwani darasani wanakaa wanne wanne kwanye dawati moja, so watagelezeana.
Mimi nna uhakika mtiani wenyewe, neshno, hawafanyii chini, sasa sielewi kwa nini hao walimu wasiwape homework za kutosha wanafunzi wengine woote, ili darasa la saba wafanye mtihani kwa raha, maana moko ni kipimo cha mtihani wa kweli, hapa mwanafunzi hawezi hata kupim spidi yake, na lazima yaje matokeo mabaya, ambayo yanaweza kuvunja moyo wanafunzi wengine wakaona wao ni wa kufeli tu.
Huu uamuzi wa walimu hawa umenisononesha sana.

2 comments:

Anonymous said...

Inasikitisha lo

Anonymous said...

very sad news ni bora wangeachwa wagelezeane kuliko kukaa chini namna hiyo. Nashangaa sana hivi wako wapi watu wanaoshughulikia haki za watoto Tanzania??? hivi hawaoni hizo child abuse kweli??? au wanadhani kuchapa fimbo tu ndio child abuse?? sina mtoto lakini ninasikia hasira sana na kitendo hicho cha uonevu wa watoto.