Tuesday, June 2

Daktari Bingwa Mtoa Mimba Auawa

Dr George Tiller
*****
Daktari bingwa wa kutoa mimba kubwa, Dr. George Tiller amepigwa risasi na kufa hapohapo, alipokua anahudhuria misa kwenye Kanisa la Kirutheri la Reformation Jumapili hii, huko Marekani.
Kwa muda mrefu Dr Tiller alikua anatafutwa na watu wanaopinga utoaji mimba nchini marekani, na mara kwa mara yeye na familia yake wamepokea vitisho mbalimbali kutokana na kazi yake. Mkewe alishuhudia mauaji hayo akiwa amesimama anaimba kwaya mbele ya kanisa.
Br Tiller alikua anamiliki klinik moja kati ya tatu tu nchini Marekani ambazo zinatoa mimba iliyopita wiki 21, ila mimba hizo ziliku hazitolewi kwa sababu ya kutoa mimba tu, zilikua na sababu zake.
Dr Tiller alikuwa akiamini kwamba akina mama ambao imeshaonekana kuwa watoto wao ambao bado hawajazaliwa wana ulemavu uliopitiliza au magonjwa mabaya sana wana haki ya kuamua kutoa au kutotoa mimba.
Na kwa sababu matatizo hayo mara nyingi yanagundulika mimba ikishakua kubwa, ndio maana Dr Tiller alikua anatoa mimba ambazo ni kubwa sana, kitu ambacho ni hatari kwa mama mjamzito, na ni madaktari wachache kama yeye waliokua wanakiweza.
Kutokana na kazi yake hiyo Dr Tiller alishapigwa risari kwenye mikono yote miwili mwaka 1993 na klinik yake, Women's Health Care Services, ilishapigwa mabomu mwaka 1985.
Kutokana na hayo, Dr Tiller alikua anatembea na walinzi na madirisha ya klinik yake yalikua hayapitishi risasa, lakini wauaji hao walimpata kwenye sehamu ambayo hakutegemea kabisa, kanisani. Pia cha ajabu zaidi ni kwamba, hawa waaliomuua daktari huyu wanajiita pro-life (yani wanahamasisha watu wasitoe mimba kwa sababu kila mtu ana haki ya kuishi).
Sijui wadau mnaonaje kuhusu hili, ila mimi binafsi sijapenda, ukizingatia huyu dokta alikua hatoi tu mimba kwa sababu zisizo za msingi, sababu zake zilikua za msingi kabisa.

*****

Hapa kwetu kutoa mimba ni kosa la jinai, ingawa ni ukweli usiopingika kwamba wasichana wengi wanatoa mimba kila siku, na wengine wanakufa au kupata matatizo ya kiafya ambayo yanawafanya wasije kuzaa tena maishani mwao.
Hili suala limewagawanya watu kwenye makundi matatu makubwa, (ingawa kuna mengine madogodogo):
  • Watu wengi wanapinga kabisa utoaji mimba kwani wanaona kuwa kutoa mimba ni dhambi kubwa kama kuua, hivyo isihalalishwe kabisa.
  • Baadhi ya nchi wanaruhusu hadi mimba ya wiki 12 (ambayo ni kidaktara inakua bado ni salama kutoa) ila zaidi ya hapo ni kosa, na wanaounga mkono hili wanasema sababu ni kwama mtoto anakua bado hajaumbika vizuri.
  • Na kuna wachache wanaoona kutoa mimba yeyote ile ni sawa, na wanaona kutoa mimba ihalalishwe.
Wadau mnaonaje?
Piga kura hapo kulia...

3 comments:

Anonymous said...

Mie napinga utoaji wa mimba kabisa! hapa nilipo natafuta mtoto kwa hali na mali ila bado sijabahatika,sijawahi kutoa mimba na wala sitadhubutu kufanya hivyo maishani mwangu..ee mwenyezi Mungu nisaidie!!

Anonymous said...

naona jibu la swali hili linaweza kujibiwa vizuri na yule mtu aliwahi kutoa mimba, yani aseme inakuwaje au ni nini aliwaza hadi kufikia kitendo hicho maana anaweza akawa na sababu ambayo kila mtu atakubali uhamuzi huo. Binafsi kwa imani yangu naamini kutoa mimba ni dhambi sawa na kuua tena kwa makusudi kabisa lakini pia kuna situations ambazo nikifikiria naona kama vile zinaweza kuhalalisha utoaji mimba fikiria mtu amebakwa na mtu hata hamjui ina kuwaje hapo?? ila sikubaliani na utoaji mimba kwasababu mtoto atazaliwa mlemavu kwasababu hata walemavu ni binadamu kama binadamu wengine wanayo haki ya kuhishi.

Anonymous said...

Mungu akujaalie upate mtoto mwaya, God is able, hakuna lisilowezekana.
Mimi pia napinga utoaji mimba.