Tuesday, June 9

Nipo Kwenye Kiji-shule...

Wadau msione kimya, nilikuwa safarini tangu Ijumaa iliyopita, nimefika jumamosi, na nilikua sijatulia, sasa ndio nimetulia na kuweza kupost kwenye glob yetu...niko Berlin, naongeza maujuzi kwenye multmedia and online journalism ( yanahusiana na hayahaya nnayoyafanya hapa) so nikirudi ni moto mbele...lazima glob iboresheka, na naplan kuipeleka to another level...
Hapo niko kwenye bustani ya mawaridi kwenye park kubwa hapo Berlin...
Msiache kuendelea kutuma picha za wadau, maana libeneke linaendelea hukuhuku...

8 comments:

Anonymous said...

yaani siku mbili tu umeshang'aa kweli huko ni ulaya

anti didy

Anonymous said...

Tunasubiri kuona pia watoto wa Berlin. Mwanao umeondoka naye? Kama siyo, je utafanya mikakati gani kuhakikisha kuondoka kwako hakumuathiri? Mdai wako. Tunakuombea.

Anonymous said...

Nimekosea kuandika mdai badala ya Mdau wako. Tunakuombea.

Anonymous said...

Nakupongeza kwanza kwa kupata fursa hiyo.
Ila jee na X upo nae? yaani ikiwa haupo nae inanikumbusha na mimi siku nilipomuacha Hosam,inauma sana lakini ndio hivyo tena,ila mimi nikuchekeshe kitu kimoja,mwezi wa March ilikuwa Hosam tayari tayari hatua zote za kufika nilipo mimi,lakini wapi Bibi yake alipoona kweli imedhiri akasema hawezi kuishi bila ya mjukuu wake,amekataa kabisa ikabidi tumkubalie.
Ila Mola akijaalia Hosam atakuja kupokea yeye mwenyewe shahada ya mamii wake mwakaniii mwezi kama huu,mmhh!! ni mbali??????

Maggie said...

My sis J,,, congrats, haya itabidi utuwekee mada hapo juu ya jinsi ya kuwa handle watoto tukiwa masomoni kama umemuacha, je utakaa muda gani dia?????

wishing u all the good things

Anonymous said...

he wewe uliyeandika ujue hajaenda na mwanawe amekwenda masomoni jamani mtoto amekaa na babake.

anita said...

mzima? karibu sana geneva maana hapo karibu!

Anonymous said...

jiang kumbe uko bomba hivo, hebu badili picha yako hapo juu, mimi siipendi,. Please usimind ni mtazamo tu, we ukirudi piga picha ingine na X wako, utatoka bomba. Ila dada ume maintain. Huyo X alikaa kwenye tumbo gani jamani? unakula nini na mimi nile au nimazoezi gani unafanya na mimi nifanye? anyway i like you, na blog yako, very natural, keep it up