Wednesday, June 10

Wadau Mmependelea...

Baada ya kupitia comment zotee ka makini inaonyesha kuwa wadau wengi zaidi wanaona tuko 50/50, yani Xchyler amejitahidi kuwa mtoto mzuri na kuhakikisha ametuchanganya waote wawili, au kama kaka yangu Mwaipopo alivyosema, itakua akija kwetu wanasema amefanana na wajomba, akienda kwa baba wanasema amefanana na baba.
Lakini wengine wengi tu wamempendelea Sixtus na kusema yeye ndio ana damu kali zaidi, yani hamuwezi amini, wawili tu ndio wamesama ni mimi nna changu kidogo!
All in all, asanteni kwa kuamua ugomvi huo, na kwa sasa mshindi keshapatikana, ila round ya pili ni mwaka kesho, maana kuna wadau wa kutosha wamesema tusubiri hadi afikishe miaka miwili, na mpambano utapamba moto akizaliwa baby number last, Mungu akijaalia miaka miwili ijayo.

4 comments:

Anonymous said...

mmependeza baba na mwana. nakuonea huruma X utakaa miezi kadhaa bila kumuona mama yako, naye sijui huko kama masomo yatapanda bila mwanawe.

maulid

Anonymous said...

WOW! NOW THAT'S A GREAT DAD! BABA X PLEASE KEEP UP THE SPIRIT. UPENDO WA BABA KWENYE FAMILIA NI MUHIMU MNO KATIKA KUJENGA FAMILIA BORA

Anonymous said...

MAMA X MI NIMEZIA PAMBA ZA MWANAO ESPECIALLY RABA JAMANI

Anonymous said...

huyu ingependeza kama mngemwita Liwilindu/ Livilindu. au hilo sio jina la kipekee? naamini Six analipenda, au ndio wewe ulikataa hilo jina. hilo jina mie nimejaribu kulitatufa kokote sijalipata zaidi ya Liganga.