Tuesday, September 22

Komunio ya Lisa

Huyu ni binamu wa X. Anaitwa Lisa Mapunda, yeye alipata kumunio ya kwanza siku X alipobatizwa.

Huko kwa bibi wa Mbinga, komunio ya kwanza au kipaimara ni sherehe ya nguvu sana, hata sikutegemea!
Mdau mwenye sherehe lazima abebwe, aidha mabegani au kwenye pikipiki kama hivi, yani sehemu atakayoonekana na watu, hata kama kuna gari, gari litambeba baadae.

Hapa Lisa amabebwa na baba mkubwa, na wapambe tulikua tunasindikiza nyuma.

Afu ukifika home ndio unaimbiwa kama hivi, si mnamuona X anashangaa shangaa hapo nyuma akiwa amabebwa na anko.

Pilau na mapochopocho mengine yalisindikiza sherehe... ambayo mwenyewe Lisa aliifurahia sana.

1 comment:

Anonymous said...

huko hata ndoa ni lazima mbebebwe kidogo, ni utamaduni wetu wadau wa huko. dar tunaiga mambo mengi, ukitaka arusi ya kiutamaduni zaidi nenda kijijini huko kuna raha zake!!