Friday, September 18

Suprise Ubatizo...

Tulipokwenda kwa bibi Litembo yalitokea mangi, ila kubwa kuliko ilikua ni ubatizo wa Xchyler.
Ndio, tuliamua, baada ya sherehe ya harusi kuwa Dar, basi ya ubatizo iwe huko, maana tulivyofika ilikua jumapili yake ya ubatizo, kwa hiyo babu wa Litembo, Mzee Mapunda, akatumia cheo chake cha ukatekista kufanya mjukuu aingie kwenye list ya wabatizwaji kabla hawajafunga jalada Ijumaa jioni.
Kwa hiyo mdau akabatizwa Jumapili ya tarehe 06 mwezi huu kwa jina la Xchyler Jace Mapunda katika kanisa la Familia Takatifu, Parokia ya Litembo , alibatizwa na Padra Joseph Ngahi.

Xchyler alileta vituko vingi kanisani, pamoja na kupiga kelele kuwasaidia waimbaji na makofi mengi tu.
Akabatizwa kwa maji, alishtuka huyo, maana huko ni baridi afu hayo maji huwa yanakaa kwenye mtungi, so pata picha.

Baada ya kumwagiwa maji, X alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa.

X ndio alipanda alitarini kuwakilisha wabatizwaji wengine kwenye process kadhaa zilizofuata, maana yeye ndio alikuwa mdogo kuliko wote.

No comments: