Monday, September 21

X na Mbwa


Kwa bibi wa Mbinga kuna mbwa. Sasa mdau X alikua anapenda sana kuwachezea, anawakimbiza, anawavuta, anawapigapiga, anawatisha kwa kuwangurumia, yani ni utundu uliopitiliza. Uzuri mbwa wenyewe ingawa hawamjui walikua wapole sana kwake, yani hata hawakuwahi kumbwekea.
Hapa alikua anamtoboa jichoni mbwa huyu. Kwa mbali ni bibi wa Chang'ombe akiangalia kwa makini.

Hapa anampiga, piga kichani.

Anamkagua miguu.

Alivyoona mbwa ametulia tu akaamua kuanza kuangalia maeneo mengine ya kufanya utundu.
Hadi leo nimeshindwa kuelewa, maana inaelekea kama vile X alikua anadhani hao mbwa ni toys tu, maana nyumbani ana toys za mbwa wanaobweka na kutembea, sasa naona alikua anashwangaa kwa nini hao hawabweki kama wa nyumbani.
Na nnavyomjua, yeye anajua kila toy lazima kuna sehemu ukibonyeza au ukipiga inatoa sauti, sasa naona alikua anatafuta kwa kubonyeza hao mbwa watoe sauti.

2 comments:

Anonymous said...

jamani x kanichekesha mpaka basi! ah huyu mtoto kiboko, nimemkubali kwa utundu!salam kwa bibi wa litembo na wa chang'ombe!

Anonymous said...

x jamani nae ni mtundu sana.namtamani akae kwangu acheze avunje glass zote