Wednesday, December 31

Mdahalo Unafungwa: Watoto Kunyonya Vidole

Xchyler akiwa na bibi yake, kama kawaida kidole kwa mdomo.
***
Leo tunahitimisha ule mdahalo wetu uliodumu kwa takribani wiki tatu na nusu kwa maelezo ya kitaalam toka kwa Dr Sima. Nimezingatia ushauri wa mtaalam. Stay tuned as kesho tunafungua mpya, uwahi ukiwa wa moto.

***
UNYONYAJI WA VIDOLE.Unyonyaji wa vidole kwa vichanga na watoto wadogo ni jambo la kawaida. Karibu asilimia 80% ya watoto huyonya vidole.Inasemekana kuwa tabia hii huanza tumboni baada ya wiki kumi na tatu za ujauzito na uendelea mtoto anapozaliwa ingawa wazazi wengi hugundua pale mtoto anapofikisha umri wa miezi miwili mpaka mitatu.
Wapo watoto ambao tabia hii huanza baada ya kuzaliwa. hata hivyo hakuna tafiti iliyoweza kugundua kama tabia hii ni ya kurithi(genetic) na hivyo kuendelea kuhakiki kuwa hutokea kwa mtoto yeyote hata kama kwenye koo alizotokea hakuna au hakukuwahi kuwa na tabia hiyo.
Tafiti nyingine za kisayansi zimeonyesha kuwapo na sababu za kifamilia zinazoweza kusababisha tabia hii itokee kwa mtoto zaidi ya mmoja kwenye familia moja kama ntakavyoelezea hapo chini.
Unyonyaji wa vidole hupungua au kuisha kabisa pale baada ya miezi 8 mpaka 9 ,japokuwa watoto wengi huendelea hasa wale ambao sababu kuu ya unyonyaji ni kujifariji(comfort) wakati wanaposikia njaa,hasira,woga,,usingizi,bored kuiga kutoka kwa ndugu ama rafiki zao n.k Hivyo kutokana na sababu hizo mtoto wa malezi yoyote na familia yoyote anaweza kuwa na shida ya kumfanya atake kunyonya kidole,kwani sababu nyingine zinahusisha hisia za mtoto mwenyewe na si familia au mzazi.

MATATIZO YATOKANAYO NA TABIA YA KUYONYA VIDOLE.
Kunyonya vidole kwa muda mrefu hasa kidole gumba, humsababishia mtoto matatizo ya mpangilio mbaya wa meno kwani husukumwa kwenda mbele au kujipanga vibaya na hivyo kuathiri muonekano wake. Mpangilio mbaya huweza kujirekebisha wenyewe iwapo mtoto ataacha kunyonya vidole ingawa tabia hii ikiendelea mtaalam wa meno (orthodontists) atahitajika kumrekebisha..
Pia kutokana na kunyonya vidole mtoto atapata tatizo la matamshi,na viungo vta mdomo kama ulimi kutoka nje wakati wa kuongea.
Hata hivyo tatizo kama kukosa akili au kupunguza concentration kwenye masomo kama wanavyoamini wamama wengi limepingwa na wataalamu wengi.
Unyonyaji wa kidole haupunguzi saizi ya kidole kama inavyoaminiwa na wengi pia bali hufanya ngozi ya kidole kusinyaa na kuwa ngumu ama nyeusi na hii huisha pindi tabia inapokoma.

Kama nilivyotangulia kusema unyonyaji wa vidole si hatari kama mtoto ataacha kunyonya atakapofikisha miaka tano au pale atakapoanza kuota meno ya utuuzima ambayo ni kati ya miaka 4-6 inategemea na ukuaji wa mtoto kwani wengine huwahi na wengine huchelewa lakini si zaidi ya miaka 6 .
Kikubwa cha kuzingatia hapa ni mazingira ya usafi kwani ni rahisi kwa mtoto kupata maambukizi ya bacteria na minyoo.watoto wanaonyonya mara kwa mara baada ya miaka minne au mitano na kuendelea wana hatari ya kupata tatizo kla mpangilio mbaya wa meno,muonekano mbaya wa sura na hata matatizo ya kuongea vizuri.
Mara nyingine unyonyaji wa vidole unatokana na matatizo ya kihisia (emotional problem) na hivyo kulazimu mtoto aangaliwe kiutaalamu zaidi. Hata hivyo watoto wengi huacha tabia hii njia rahisi za kuzuia unyonyaji huo zinapotumiwa

JINSI YA KUONDOA TABIA HII.
Watoto wanaonyonya vidole wanaweza kuachwa tu waendelee kunyonya kwani wataacha wenyewe isipokuwa kama unyonyaji huu utaendelea baada ya miaka minne .utaanza ghafla baada ya miezi kumi na ukiambatana na kuvuta nywele
Njia zinazosaidia kutibu tatizo hilo ni
1. Kumueleza mtoto kwa lugha nzuri na ikibidi kumuahidi zawadi nzuri pale atakapokubali kuacha tabia hiyo.
2. Kumpeleka shule kwani kunaweza kusababisha aone aibu na kuacha hasa pale atakapo taniwa na wenzake.
3. mzazi kufuatilia kwa makini sababu inayomfanya mtoto anyonye kidole na kuiondoa.mfano kumpunguzia mda mwingi wa kuwa bored au kunyonya vidole ,kuweka mbali vitu vinanyochochea unyonyaji wa kidole mfano blanket au mashuka.
4. Pia mzazi anaweza kutumia vitu kama bandage na kumuelewesha mtoto kuwa hiyo si adhabu bali anamsaidia ili meno yake au sura isiharibike,mzazi anaweza kutumia vitu ambavyo si sumu au vichungu kama finger nail polish, pili pili,asubuhi,kabla ya kulala au mtoto anaponyonya.
Ingawa njia hii inashauriwa iambatane na zawadi pale atakapoacha ili isiwe kama adhabu kwa mtoto.

Iwapo vyote vitashindikana basi mzazi au mlezi asisite kuwaona madaktari wa afya ya meno ya watoto au daktari yeyote wa meno aliyekaribu nae kwa msaada zaidi.
By Dr. Sima (DDS).
***
Thanx Dr Sima.

5 comments:

Anonymous said...

how can you write a so cool blog,i am watting your new post in the future!

Anonymous said...

dada j naomba email ya dr sima nina tatizo kubwa la mtoto wangu .asante

Anonymous said...

Different people have different life, different people have different interpretations of human life, you may pay more attention small links, so you have style!

Anonymous said...

It seems my language skills need to be strengthened, because I totally can not read your information, but I think this is a good BLOG

Anonymous said...

mh be careful na idea zako pilipili huku nilipo ni big issue akiweka jichoni je ? utaenda police bila kujijua hiyo ni child abuse mama point taken