Monday, January 12

Mdahalo: Housegirls Tuwatendeaje?

Janeth Mushi, akiwa na kipenzi chake, Thierry Murunga, ambaye mwenyewe anasema, 'He is my world and I am so proud to be a mom'.
***
Mdau ameleta hoja hii mezani, anasema yaani housegirl hata umjali vipi analeta vituko tu au ataondoka tu. Sasa anauliza hivi mtu umtreat vipi housegirl ili asilete vituko wala asiondoke, maana hili ni janga la kitaifa.

6 comments:

Anonymous said...

Housegals jamani si wazuri sana, it is just that we cant live without them. wanakunywa maziwa ya watoto, fomula wanakunywa then wanazidisha maji , it is very bad kwa mtoto. kukuta mzuri one in ten. kama wamama we have to be xtra careful with them.

Anonymous said...

mmh, hii topic kali, mimi nna watoto wawili, miaka 5 na 2, ilibidi nichukue likizo ya dharura kwa wiki ili nitafute housegirl. kwa kweli ni janga la kitaifa, maana siku hizi kuwapata kasheshe, unatafuta hadi unachangwanyikiwa!

Anonymous said...

Hahaa Jiang Umenichekesha kuliita 'janga la kitaifa' manake ni kweli kabisa, ila nafikiri ili kuepuka matatizo tuangalie kwa nini housegirl/boy anakuwa tatizo kwetu wamama? saingine ni mitazamo duni ya housegirl kuhusu maisha, au uroho tu au wewe mama mwenye nyumba unamweka mbali humshirikishi na kummisstreat au majirani wanamdanganya au ndugu waliopo kwenye familia wanataka wooote kufuliwa nguo zao na housegirl huyo huyo mmoja, nk nk nafikiri tukifahamu sababu tukaitafutia suluhisho housegirl aweza dumu. Kwa mfano kama anakula chakula cha mtoto kama alivyosema mdau alopita, mpe chakula /matunda ale mpaka azoee aone ni vitu vya kawaida, (maybe kwao hakuwahi kula vyakula mlivyonavyo) au ongea nae ujue nini kinam-influence ili uweze ku control the source of any bad influence, ingawa nahii si guarantee manake hsgirl wengine kwa immaturity zao anaamka asubuhi anajisikia kurudi kwao akaolewe despite mambo yooote mema ulomfanyia, Kingine muombe Mungu kwa ajili ya mtu wa kukaa na mtoto wako, hii ni muhimu sana kwani hsegl ana nafasi/role kubwa kwa mtoto wako.
Mdau Netherlands

Anonymous said...

kweli in janga. ila tujaribu na sisi kina mama kuwatreat hawa housegirls kama wadogo wetu jamani. tusiwe wakali sana juu yao kwani nao ni binadamu kwa hiyo kukosa ni jambo la kawaida

Anonymous said...

mh jamani h/girl hata ukimlea kama mdogo wako huwa hawathamini yani nashimdwa kuelewa utafikiri wamesoma shule moja ya kukarahisha watu sio kweli kwamba treatment ndio tatizo,nafikiri basi tu wameshagundua wana umuhimu ndo mana wanafanya vitu vya ajabu, mi nafikiri ni ulimbukemi ndo hasa unawasumbua huwa wanajiona wajanja kwa vitu vya kijinga kabisa

Anonymous said...

Ki ukweli haosegirl/boy hawana matatizo, tatizo kubwa ni pale wanapoanza kupewa majukumu ambayo alipaswa ayafanye mama na hapo ndipo mambo yanapoanza kwenda kombo.

Kwa mtazamo wangu kama wakichukuliwa kama sehemu ya familia, wakalelewa na kuhudumiwa kama wengine, Baba hawezi kumtafuna housegirl wala mama kuliwa na Houseboy kwa kuwa kutakuwa na social distance.