Tuesday, February 24

Kumbe Hata Wavulana Wamo

Watoto wakitoka kuwapa mashada ya maua Rail Gul na mke wake, wa kiume anampa First Lady, wa kike Presida.
*****
Last week nililalamika kuwa watoto wa kiume huwa hawapewi nafasi hii, kuna mtu akaninong'oneza kuwa hata wa kiume huwa wapo, ila mara nyingi picha inatoka ya wa kike sababu wa kike ndio anampa mwanaume, na marais wengi ni wanaume, kuona picha ya mtoto wa kiume anatoa maua labda tumsubiri mama wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf akitutembelea, na ntatafuta nafasi handsome boy wangu apate nafasi hiyo adimu.
Afu kwenye ile picha ya Banda kuna mtu amemtambua yule mtoto,...ukitaka kujua ni mtoto wa nani soma coment za picha ile...afu kama kafanana nae vile...?
Ila bado hatujui hawa watoto wanatokana na mchakato gani, na sisi tungependa wanetu watokee jamani.
(Picha via Anko Michu)

No comments: