Saturday, February 28

Sare Sare Maua - X na Brian

X akiwa na nguo zake, hizi alipewa na aunty wake flan hivi anaitwa Love (Irene Peter) alivyokua mchanga, zikaanza kumtosha alipofika miezi sita kama kwenye hiyo picha. Ila mwanangu hapendi cap, ukimvalisha anaivua, so huwa simvalishi na cap yake.

Hii picha ya Brian Kamugisha akiwa na nguo kama hizo nimeipata juzijuzi tu, naona tofauti ni randi za hizo nguo, ambayo nimeiona baada ya kutaka kuzitumia, nilidhani zinafanana kila kitu. Naona Brian mtoto mtulivu, amevaa ca bila tatizo.

*Kwa jinsi watoto wetu walivyopendeza na hizo nguo, inabidi Nike wawatumie kwenye matangazo, haki ya nani tena.*1 comment:

Anonymous said...

Kweli watoto ni raha tupu. Nawapongeza wamama wa hawa watoto kwa kuwavalisha viwalo safi. Siyo mama unatinga viwalo bab kubwa halafu mwanao anavaa mitumba.