Saturday, March 7

Aurelia Amepania Kutoachwa!

Hii ni story ya safari ya Aurelia, baada ya kuona mama yake anataka kuondoka na kumuacha akaamua achukue hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo, ambapo mama nio atabaki home, mtoto anaondoka na vitendea kazi vyote vilivyoko kwenye pochi.
Kwanza akachukua pochi na kwenda nayo nje.Akaanza safari mwenyewe, huku akiangalia nyuma kama kuna watu wanamfatilia.
Alipofika getini, akaamua kufungua geti mwenyewe bila kusubiri msaada wa mtu yeyote.
Confused! geti limegoma kufunguka.
Dada anajaribu kumconvince aachie pochi, ili mama aende anakotaka kwenda, ila, mmmh, inakua ngumu kumwingiza mkenge binti huyu.

4 comments:

Anonymous said...

nice work kwa aliyepiga picha, kiukweli nimependa mtitiriko wa tukio zima la binti huyu wa kizazi cha sasa. Yangumacho

Anonymous said...

inauma kweli kumwacha mtoto jinsi hii. Lakini utafanyeje? Kazi pia ni muhimu kwa maisha yake. Ndiyo maana wakati mwingine akina mama tunachelewa kufika job kwani hulazimika kuacha tumewabembeleza, kuwakiss na hata kuwalisha chakula watoto.

Anonymous said...

mh mtoto kaniacha hoi ha, jamani ni vituko! halafu ana mapozi mazuri ya ubebaji pochi, yupo juu!

Anonymous said...

Jamani na yeye anataka kwenda kazini kila siku tu mama anaenda kazini, leo zamu yake