Tuesday, March 24

Lishe ya Mtoto Baada ya Maziwa-Utajuaje Yuko Tayari?

Thierry Mukanda, anataka atumbukize vidole vyote mdomoni, dalili ya kutaka chakula kipya?
*****
Utajuaje Kama Mwanao Yuko Tayari Kwa Vyakula Vingine?
Mwanao atakupa dalili za wazi kabisa akiwa tayari kuanza kula vitu vingine zaidi ya maziwa tu kama:
· Kukaza shingo: Ili uweze kumlisha vitu vingine zaidi ya maziwa tu lazima mtoto awe na uwezo wa kukaza shingo na kusimamisha kichwa vizuri.
· Kuacha kutema chakula: Kwa waliowahi kuwapa chakula watoto wao watalijua hili, mtoto akiwa mdogo sana huwa hana control ya viungo vyake vingi, kama ulimi, ukimpa chakula unatoa chakula nje badala ya kupeleka ndani, so kuweza kupeleka chakula ndani ni dalili kuwa anaweza akaanza kula.
· Kukaa vizuri akiwa anashikiliwa au ameegemea mwilini kwa mtu aliyemshika ni kitu muhumu kuhakikisha kuwa ataweza kula na kumeza akianza kulishwa.
· Kutafuna tafuna: mtoto mwingina utakuta anatafuna tafuna tu kila saa, wakati yeye anakunywa maziwa tu, ujue huyo anakuonyesha kuwa anataka vyakula vizito kama uji.
· Kuongezeka uzito: watoto waliozaliwa kwenye uzito wa kawaida wanakua tayari kula wanapokua na uzito mara mbili ya ule aliozaliwa nao, mfano kama alizaliwa na kilo tatu sasa ana kilo sita, maana yake mwili wake unahitaji zaidi ya maziwa peke yake.
· Mjaa kali: hata umnyonyesha usiku kucha na mchana kucha hadi maziwa yanakauka mtoto hashibi, mmmh, hapo ujue hiyo hoteli yake unayotembea nayo haimtoshelezi tena.
· Kutamani mnachokula wakubwa: mtoto akiwa anawaangalia angalia wakati mnakula kama anatamani hicho chakula maan yake anatamani kweli, maana ameshaanza kujua harufu za vitu vitam.

Xchyler’s Experience
X alikua ametimiza mengi ya hayo masharti mapeema, maana alidouble birth weight yake akiwa na mwezi mmoja na wiki, alizaliwa na kilo 2.8 clinic ya mwezi wa kwanza alikua na 5.4, ila kushiba alikua anashiba, mama yake nilikua na maziwa mengi sana, alikua ananyonya na mengine ilibidi nimwage, ili nisielemewe na uzito na maumivu.

3 comments:

Anonymous said...

Mwanangu ametimiza miezi kumi hivi sasa, lakini katika kipindi cha wiki mbili sasa amekuwa akikataa kula, sababu sielewi na ila kiafya yupo bomba, leo asubuhi wakati mama yake anampa uji katapika kidogo sijui atakuwa na tatizo gani. Baba Big Psalm

Anonymous said...

Pole baba Big Psalm,baby anaweza kuwa ni meno tu yanamsumbua ndio walivyo watoto wako on and off kwenye maswala ya milo, kutapika anaweza kuwa alikuwa ameshiba mama nae analazimishia hivyo ikachukula Psalm kutapika kingine ni kwakuwa watoto age hiyo wanataka kutia kila kitu wakionacho mdomoni labda alitia mdomoni kitu ambacho kichafu hivyo akawa amepata kainfection kadogo au pia kutapika pia labda ajisikii vizuri (homa).

Anonymous said...

Thanx, ni kweli Psalm meno mawili yale ya mbele ndio yametoka, inawezekana hizo zote ni sababu hasa kula viti vichafu. Ila Psam ni mjanja na wakati mwingine kumdhibiti inakuwa ngumu, unaweza ukawa unmekaa nae akazunguka akapita chini ya meza akahamia upande wa pili then mbio hapo anatambaa na kusimama sijajua akianza kutembea. I love my baby boy. Thanx for advice