Wednesday, March 25

Lishe ya Mtoto Baada ya Maziwa-Kumuanzishia Chakula/Uji

Aurelia akijitahidi kula mwenyewe, sio kusubiri watu wamlishe.
*****
Mtoto Anapoanza Kula
· Mpe mtoto chakula laini ulichomwanzishia, kijiko kimoja au viwili vya chakula mara mbili kila siku. Ongeza uzito, kiasi na aina za vyakula taratibu kadiri mtoto anavyokua.
· Kwa kuanzia, chakulacha mtoto kiwe laini, lakini kisiwe chepesi au cha majimaji sana. Kadiri mtoto anavyozoea kula na kutafuna, aanze taratibu kula vyakula vilivyopondwa na vigumu kiasi. · Please, usichanganye vyakula vingi mwanzoni, mtoto anaweza akawa na allergy na kimojawapo na usijue ni kipi, ukabaki unahangaika kila hospitali. Anza na kimoja tu kinatosha akizoeazoea unaongeza kutu kindine, then unasubiri kama wiki uone unaongeza kingine.

Mchanganyiko Wenyewe
· Mwanzo: Uji wa aidha mahindi au mchele tu, nashauri usage unga wa mahindi mwenyewe na yasikobolewe au kama unaweza kupata unga wa mahindi yaliosangwa bila kukobolewa its ok.
· Then boresha uji wa mtoto kwa kutumia, karanga ili mtoto apate mafuta.
· Toka hapo utakua unaongeza vyakula kadri unavyojisikia, ila usiongeze mchanganyiko ukawa mwiiingi, hadi haieleweki faida yake ni nini, mfano, mchele na mahindi vyote ni wanga, sio lazima vichanganywe kwenye uji mmoja, ni kama kula wali na ugali kwa pamoja.
· Mtoto anaweza kukataa chakula flani, au hata uji wenyewe akawa hautaki, usimlazimishe, jifanye kama umekisahau, afu mpe tena baadae, au kesho yake anaweza akakubali.

Xchyler’s Experience
Xchyler namchanganyia mahindi, maharage ya soya yaliyochemshwa kidogo na kuanikwa juani yakakauka na dagaa wa ziwa nyasa (aina ya dagaa ni baba yake aliyeleta utaalam, anasema eti dagaa wa ziwa nyasa wanafanya mtoto awe na akili, ila dagaa wowote wakavu wanafaa).
Hivyo vyote vinasagwa mashineni, hii ni kazi maalum ya Bibi yake (what will I do without her?). Halafu nyumbani tunasaga karanga mbichi, ambazo zinakua pembeni, hazichanganywi, as kwranga ni rahisi kuharibika na kuleta wadudu, tunakua tunaongezea kidogo tu wakati wa kupika.
Ukiweka maharage ya soya hakikisha uji unachemka sana, yake hayaivi mara moja. Pia kwenye mchanganyik0 dagaa wasiwe wengi sana, si mnajua harufu ya dagaa, mtoto anaweza asiipende.
Mezani tunamuongezea chumvi na sukari kidogo (huo nao ni utaalam wa bibi, mi kwa kweli huo mchanganyikoa sijawahi kuuonja hata sijui una utam gani, maana mi kitu kikishachanganywa chumvi na sukari tu sikipendi, ila watu wengine wakila wanusifu kuwa ni mtam).
Pia tunagongea yai la kienyeji, (baba yeka pia amesema hataku kuona yai la kidhungu kwenye uji wa mwanae, nab bibi akamsapoti, mi yangu macho tu, nawasikiliza wao).

11 comments:

Anonymous said...

Duh!!this blog is real helpful now!Big ups to all women.Endelezeni jamani, maexperience ndio yanaitajika,tuzidi kushare ideas..

Keep up the Good work Jiang.

Anonymous said...

Jamani tusaidiane hapa jumvi na sukari sio nzuri kwa watoto wadogo kama mnaweza kuwatengenezea vyakula bila sukari na chumvi itapendeza zaidi na itasaidia kutunza afya zao unaweza kutumia matunda kama ndizi za kuiva ukaponda na kuweka kwenye uji uliokaribia kupoa na mtoto akanywa vizuri kuliko kuwatafutia watoto magonjwa yanatokana na chumvi na sukari na pia kuna effects kibao kwa matumizi ya sukari na chumvi kwa watoto hasa chini ya miaka kumi

shamim a.k.a Zeze said...

Thanks..Jiang hili somo limenikunaa mnoo naomba upige picha hivyo vyombo vya kulia watoto kina sie tujiandae

Nikuchekeshe..juzi nimebebeshana na Iqra..twaenda hospital mwanangu anajinyonganyonga...Gesi ndo tatizo...na kwi kwi inamsumbua nimekatazwa nisimpe maji zaidi ya kunyonya ziwa tu

sijui ulishaongelea hayo au...ila doc alisisitiza ziwa la mama is the best..jamani hata maji???!!

Anonymous said...

ASante dada kwakweli nimejifunza mengi sana apa, aya ndio mambo tunayahitaji sana, asanteni kwa kutuelimisha sisi wengine

Anonymous said...

Mama Igra kujinyonganyonga kwa mwanao ni kujaa kwa gesi tumboni hili tatizo ni common sana kwa watoto wa kiume mimi mwanangu alikuwa nalo ila sio common sana kwa mabinti mpatie mwanao maji ya uvuguuvugu kabla hajanyonya then mnyonyeshe fanya hivyo kila anapotaka kunyonya utashangaa jinsi haya maji yanavyofanya miujiza kuna dawa pia ila kwa upande wangu sishauri sana habari hii ya dawa kwa sababu sio nzuri kwa watoto ila kama unahitaji kuijua dawa hii ya kuondoa gesi inaitwa infacol.

Anonymous said...

mama iqra anaweza pia kutumia gripe wwater ndio ilimsaidia mwanangu.maji sio mazuri

shamim a.k.a Zeze said...

Shukran anony...yeah dawa nilipewa iyo iyo...japokuwa naona nayo haisaidii coz bado anajinyonga tu...sasa hayo maji ntampaje na ndo nimeambiwa maji yapo katika maziwa ya mama...ntajaribu hilo...shukran

mama nashdigo said...

mambo shamim, mama iqra jina la mwanao zuri najua hilo ni neno lililo kwenye quraani ambapo kwa kiswahili ni soma. nilifurahi kusikia umepata baby. mimi ni zena chande tulikuwa wote msj, siku hizi najulikana kama mama nasri. suala la kujinyonga kwa watoto ni kawaida hiyo mama yangu, we fuata tu maelekezo ya hao wataalam wenzetu waliotangulia,hata mimi wa kwangu nilikuwa nampa maji ya uvuguvugu yalimsaidia sana natia na viglucose kidogo, watoto chini ya miezi mitatu ndio hawaruhusiwi kunywa maji wakimaanisha ya kunywa kama unavyofanya wewe, ila kwa hivyo vimaji vya uvuguvugu sio mbaya vitasaidia we jaribu kumpa

Anonymous said...

Pole sana shamim, kwanza akikisha mtoto anapomaliza kunyonyo akikisha anatoa hewa yaani (kubeua)hii pia inamsaidia kutoa gesi, pia maji hayo ya vuguvugu yanafanya kazi vizuri sana, tena mie nilikuwa namuwekea kapinch ka chumvi na sukari kidogo alikuwa analala vizuri saaana, ila najua ukiwa mzazi mtoto akawa anasumbuliwa na kitu unakuwa desparate kuangaika kipi bora zaidi, mie nikatumia pia na hiyo infacol ilimsaidia pia kwakweli, kwa hiyo grape water madoc wengi wanakataza aisee, sasa sijui. maziwa ya mama yana maji pia lakini ndio hayohayo yanayompa gesi, so its better kuwasaidia watoto wetu coz hawawezi kujisaidia, zingatia kumtoa hewa kila baada ya mlo dear.

Anonymous said...

Mama IQRA maji ni muhimu kwa binadamu lasivyo tungeshindia coca ama pepsi na maziwa ya mgando au fresh maana yana maji ndani yake kwa nini basi tunywe maji kama yanapatikana ndani ya vinywaji vingine maji yana umuhimu wake mimi nilitoa hio comment hapo juu ya kutumia maji nasisitiza mpatie mwanao maji ya uvuguuvugu kabla ya kunyonya na maji hapa yanatumika kama dawa na sio kinywaji.
Mama E

Anonymous said...

Nimefurahi sana kukutana na mambo haya, kwan nimejufunza mengi haswa kwa mwanangu mchana bado. Big up wamama.