Wednesday, March 4

X Anaumwa

X akitoka hospitali na baba yake.
Hapa nimempakata hospitali anadeka kichizi, hata babu yake alikua anamdekeza jana.
*****
Xchyler anasumbuliwa na kikohozi na mafua, jana alikua ana homa, ikabidi tumpeleke hospitali, maana dogo aliacha utundu wote akawa mpolee. Ila hakuacha kuitumia nafasi hiyo kumdekea kila mtu anayembembeleza, kama jana alikua hamtaki mtu, zaidi ya baba, mama, bibi na babu, ambaye jana amemdekaza sana tu.
Afu kama msimu wa mafua na vikohozi kwa watoto umeanza, wadau wawili watatu wameniambia na watoto wao pia wanasumbuliwa.
Nawaombea wote waugue pole, na Mungu awasaidie wapone haraka, na warudi kuwa wachangamfu kama kawaida yao.

4 comments:

Anonymous said...

Augue pole jamaaani,yaani nimemuonea huruma,ila nakushauri kitu kimoja,tusipendelee watoto kuwapa madawa haya ya hospitalini sana,mimi mtoto wangu alikuwa akisumbuliwa na mafua alipokuwa na miezi minane(sasa ni mwaka na miezi 7,na mmiss sana kwani niko nae mbali)alikuwa anasumbuliwa na mafua,basi nikampata daktari mmoja bingwa wa watoto anatoka CUBA,basi akanishauri nisipendelee kabisa dawa hizo,ila kila asubuhi akiamka tu na mchana,na jioni nimshafishe kwa maji ya uvugu vugu,then,yenye kutoa mvuke niyaweke kwenye chombo na nimuinamishie ili mvuke umpate,then nichukue mengine ya uvuguvugu niweke chumvi kidogo,then nichukuwe cotton bud nichove kidogo yale maji,nimuekee matone katika pua.
Yaani hiyo ndio dawa iliyomsaidia mtoto wangu.Na kuhusu kifua ni kwamba upate asali safi,hayo hayo maji ya uvugu vugu pamoja na kijiko kidogo unaweka asali na unamnywesha mara tatu kwa siku.

Anna said...

Jamani pole sana X kwa kuugua, na poleni wazazi kwani kuugua kwa mtoto ni taabu kwa mzazi. Natuamini Mr X kwa sasa anaendlea vizuri, Mungu awabaliki sana kwani mnapendeza sana.

Anonymous said...

Pole sana X... Vimafua mafua na vikohozi kwa watoto kwa wakati huu ni kawaida tu Mama X... Zingatia tu feni isimpate sana mtoto kwa kuwa si nzuri sana kwa watoto wenye umri kama wa X.. X ugua haraka haraka utundu urudie pale pale... Kwakuwa nikisema Uugue pole hutapona haraka M-baby...

Anonymous said...

Nimependa comment ya mtu wa kwanza, kiukweli madawa ya Hospitalini yana athari kubwa kwa watoto wadogo.

mtoto wangu huwa anapata tatizo kama la x hasa akibebwa na mtu anayetumia manukato makali kiukweli nilikuwa nakaribia kumwambia mama yake asiruhusu mtu kumbeba mtoto ila nikaona itakuwa ngumu kufanya hivyo