Thursday, April 16

Happy Birthday My Angel

Toka Hapa... Huyu ni Xchyler wangu siku ya kwanza baada ya kutoka hospitali. Alizaliwa usiku wa kuamkia siku kama ya leo, mwaka jana, mida ya saa nane na nusu usiku. Kiukweli, nilimkodolea macho usiku mzima, halafu yeye alikua ametuliaa, wala hakuamka, nikawa namgusa shavu ili at least atikisike kidogo. That was the most amaizing day in my life, hadi leo siamini kama huyu ni mtoto wangu...Being a mother is the most prescious thing in the world.

Hadi Hapa...

Xchyler juzi juzi tu, kunyonya kidole, hajaacha. Siku hizi ni mtundu sana, hadi raha, kiukweli ananipa raha na faraja kubwa sana.

*****

Nawashukuru woote wanaonisaidia katika matunzo ya mwanangu mpendwa, hasa, mama na baba yangu, & Mrs Alipo...I could never ask for better grandparents, wanavyompenda mwanangu, hadi nahisi mimi simpendi kama wao. Pia mume wangu mpenzi, Sixtus Mapunda, u r the best husband and father. Wakwe zangu, Mr & Mrs Mapunda, maombi yenu yanatufanikishia kila kitu kwenye maisha yetu, Mungu awabariki sana. Bila kuwasahau Anko zake, Alipo na Albert, asanteni kwa kumpenda mpwa wenu.

Ndugu, jamaa, marafiki na wadau wooote, akhsanteni sana.

3 comments:

Anonymous said...

Happy Birthday Xchyler!!!
Hongera wazazi kwa X kufikisha 1yr!
May the almight God grant him a long and yet happy life!!!
Mama Frida

Anonymous said...

Happy birthday X jamani mimi mchelewaji usiache kupokea salam zangu naona kama ingekuwa kwenye sherehe ningekuta watu wanamalizia kutoa viti Hongera sana mama Xkwa matunzo mazuri ya X mungu akukuzie.

shamim a.k.a Zeze said...

Hi Jiang
kwa nikupe HONGERA kwa kukuza a year si mchezo mie ndo kwanza siku 46
...nilikuwa nakatiza fasta baada ya baby Iqra kulala nikakuta hii post...hakika ni nzuri na mie naomba niweke haka kalink ili wadau kiwasaidie kwani mimi ilinisaidia saana ni maoni toka kwa wadau wangu wa 8020 fashions pindi walipopata taarifa nina tarajia na wakanipa maujuzi

http://8020fashions.blogspot.com/2008/12/raha-iliyoje-kuitwa-mama.html

nb: nilikuwa nasikiliza kipindi cha afya ITV ambapo alikuwepo dr Massawe: Alisema never mtoto kuvalishwa kanga zilizochangaa as yeye ni mpya mnamuambukiza mtoto bakteria jamani...hivyo kina mama tutumie kanga mpya mzifue na kupiga pac.