Wednesday, April 15

Mahitaji ya Awali ya Mtoto - Kuoga

Dalvis Mlingi akijidai kwenye bathtub yake.
*****

KuogaBeseni: kwa ajili ya kumuogeshea
Vitaulo: hivi sio vile vinavyoshikwa barabarani na wamachinga, kuna maalum kwa ajili ya watoto, vipo kwenye maduka ya watoto.

Sabuni: binafsi ni shabiki wa Johnson’s No More Tears (ni ya maji). Inafaa sana mtoto ambaye hajui kufumba macho, na hataki kupitwa na chochote kama X, maana mapovu yake hayaumizi macho.
Mafuta: watu wengi wanapenda mafuta ya nazi, binafsi sijawahi yatumia, ila walioyatumia wanasema ni mazuri sana. Siku hizi wala usihangaike kutafuta mtu wa kutengenaza wala genge linalouza, yapo spesheli kwenye maduka ya watoto, na tena hayana harufu kali.

Poda: poda inatumika ili mtoto anukia, ila pia kumfanya mtoto awe mkavu na apate kujisikia vizuri baada ya kuunguzwa na mikojo au uchafu mwingine baada ya kumsafisha na kumbadilisha.

Taulo: nunua mataulo ya watoto kwenye maduka ya watoto, yao ni malaini.

Baby Gear
Kiti Cha Gari: sina uhakika na hapa Bongoland, ila najua nchi nyingi zilizoendelea hata mtoto aliyetoka kuzaliwa lazima awekwe kwenye siti yake (hii inaweza ikawa tofauti na ya watoto wakubwa kidogo au ikawa unaweza ukaigeuza mtoto akikua). Hii ni kwa usalama wa mtoto. Hata kama hutatumia siku ya kwanza ni vizuri kuwa nacho kwa siku zijazo.
Stroller: Hii sio lazima, maana mji wetu huu kuna sehemu chache sana za kutumia. Ila kama unapenda kutoka na mwanao, (sehemu kama mlimani city, slipway…) na akishaongezeka uzito, inakua kazi sana kumbeba mkononi, so kama mfuko unaruhusu why not? 

2 comments:

Anonymous said...

I daught juu ya hiyo beseni ya mtoto ya kuogea, it is very dangerous, kwani hakuna za chini ni mpaka awe juu hivyo??? any way sijui wenzentu huko tanzania mnaonaje juu ya hili

Jiang said...

mabeseni ya chini ndio yanayotumika sana...hili la juu nadhani linataka watoto watulivu na umakini wa hali ya juu kwa mtu anayemwogesha mtoto...