Tuesday, April 14

Mahitaji ya Awali ya Mtoto - Nguo

Xchyler akiwa anauchapa usingizi ndani ya kinyelamumo cha chupi.
*****

NguoUshauri wa jumla wa nguo, hasa kutoka China, nunua za miezi mitatu au miwili mbele, kwanza watoto wanakua haraka sana, pili wachina ni wadogodogo, kwa hiyo utashangaa nguo iliyoandikwa 3 monhts inamtosha mwanao wa wiki moja.

Vinyelamumo kwa kizungu onesies: hizi ni nguo za moja kwa moja, mimi binafsi nazipenda sana, zinaweza kuwa za kichupi, yani bila miguu, na pia moja kwa moja hadi miguuni zikafunika au zisifunika hadi vidole. One-piece outfits (onesies)

Soksi: hizi kwa wingi maana zinasaidia kumkinga mtoto na baridi.

Masweta: hapa bongo ni joto lakini kibaridi kidogo tu kinaweza kukupeleka hospitali, so ni muhimu kuwa na angalau pea mbili za masweta, hasa ambazo zina sweta la juu, suruali, soksi, na kofia yake.

Kofia: vikofia ni muhimu kuwa navyo, ila watoto wanaozaliwa na nywele nyingi kama Xchyler, hizo kofia zinateleza tu, wala hazikai.

No comments: