Thursday, April 16

Mahitaji ya Awali ya Mtoto: Kula & Kulala

Xchyler akiwa anatafuta kwa kutokea kwenye kitanda chake baada ya kuamka asubuhi.
*****

KulaBibs: sijui kwa Kiswahili zinaitwaje, ila najua zinasaidia mtoto asijichafue wala asichafue nguo anapokula, hata kama ni kunyonya maziwa ya mama.

Pampu ya kukamulia maziwa/breastpump: kama utaanza kuwa bize miezi michache baada ya kujifungua, hata kama ni miezi mitatu, ni vizuri ukawa nah ii mashine, ya mkono au ya umeme kama una uwezo, ikusaidie kukamua maziwa ambayo mtoto atatumia ukiwa haupo. (hii topic ntaielezea vizuri siku nyingine).

Chupa na chuchu zake:
hata kama unanyonyesha ni vizuri ukawa na chupa angalau hata moja ya dharura. Ila kama utaanza kwenda ofisini au kwenye shughuli zako na akawa anatumia maziwa yako au mengine kwa chupa, ni vizuri ukawa na hata chupa tatu. Kuna zinazouzwa box ziko nne, ni nzuri sana.

KulalaPlastic za kuweka kwenye gogoro lisiloe na mikojo.
Mashuka ya kutosha.
Mablanket ya watoto.

Samani/FurnitureKitanda: kutokana na bei bei yake na umuhimu wake baadae ni vizuri ukakinunua mapema (vingi ni kuanzia laki mbili (200,000/-)). Ushauri wa bure kina mama, siku unayoenda kununua kitanda tafuta usafiri wa kurudia nyumbani,ili iwe rahisi kukibeba. Kama una gari kubwa kifungwe hapohapo dukani, maana hao wanaume kujifanya mafundi selamara afu waharibu!

Godoro lake: Hivi vitanda haviji na magodoro, ila uatayakuta hapo hapo utakaponunua kitanda. Ni kama elfu kumi na tano tu. (15,000/-).

2 comments:

Anonymous said...

Jiang huku ughaibuni hakuna mafundi seremala wa mtaani kama bongo ndo maana nilinunua kitanda ready made lakini kwa wale walioko bongo unaweza kutafuta sample ya kitanda na vipimo vyake ukapeleka kwa fundi akakuchongea na ukapata kitu kizuri kuliko hivyo ambavyo ni ready made na ukanunua tuu godoro hii ni muhimu kwa sababu unapunguza gharama na unapata kitu roho inapenda.
labda tuu niwakumbushe wale kina mama wanaotaraji kupata watoto kitanda cha mtoto ni muhimu kama partner wako ni munywaji au analala bila kujitambua kina baba wengine wanalala wanapitiwa na usingizi na wanalalia vichanga usiku kuepukana na yote hayo mtoto kuwa na kitanda chake ni muhimu.
Kiti cha mtoto cha garini ni muhimu na hii ni kumlinda mtoto pindi aali zinapotokea kama una uwezo ni vizuri ukawa nacho.
Mama Ethan.

Jiang said...

asante mama Ethan...ila mi sipendi usumbufu wa mafundi wa kibongo, sishonagi nguo wala kuchonga kwa seramala; kama nataka kitu kwa seremala naenda kununua ambavyo walishatengeneza (vya kichina sivipendi)...nashukuru mume wangu ndio anadeal sana na hao mafundi.