Tuesday, October 13

Valle & Vice wanakula raha!


Wadau wa siku nyiiingi, Valencia na kaka yake Vicent wamepatiwa na mama yao, maana wana ugonjwa wakuchezea maji (kama X) basi mama yao, Lulu Kilonzo akaona isiwe tabu, akawanunulia hilo bwawa la plastiki, anawajazia maji humo wachezeee wee hadi wachoke.
Kwa kweli Lulu kama ulikua kwenye mawazo yangu, maana hata mi kila siku nawaza kumnunulia X, maana anavyopenda maji, we acha tu!
Nataka nijue bei yake tu, niliangaliaga zamani kidogo haikua bei mbaya sana, na kulinganisha na bwawa la ukweli, hiki kijibwawa ndio ukombozi wetu!

No comments: