Wadau wa kutosha walikuwepo, na watoto wali-enjoy kwa kweli.
MC wa party alikua Jimmy Kabwe, namsifu kaka anaweza kusherehesha watoto, maana aliwapa raha haswa, nahisi bila yeye pasingenoga sana.
Watoto walianza kwa mashindano ya kuimba, wakawa wanapanda jukwaani kwa kuimba, unajua tena watoto wa kileo, nyimbo gani wasioijua?
Huyu hapa, jina lake limenitoka kidogo, ingawa namfahamu siku nyingi, kutokana na kipaji chake cha pekee cha uimbaji, na live anaimba vizuri zaidi.
Wengi walinifurahisha, pamoja na huyu bi-dada, siku-catch jina lake, (sha ambiwa anaitwa Cassandrah, malaika wa Mange). Mrembo amemetisha kila kitu pink, na imemtoa maana alipendeza haswa.
Kama ndio hicyo, lazima wanafanya mazoezi ya kucheza nyumbani, pata picha ukiwa mzazi wao, maana lazima ni watundu tu!
Wanamuziki wengine walikuwepo ni AY, Matonya, THT, na wengine hata sijashika majina yao, ila watoto wanawajua wote, na wanajua nyimbo zao.
Kwa ufupi, palifana hasa kwa watoto.
1 comment:
hie,
huyo mtoto uliemsifia alievaa Pink ni mwanangu....anaitwa Cassandrah ..
Thanks
Mange Kimambi
Post a Comment