Tuesday, November 10

Unajua nini kuhusu sheria ya mtoto iliyopitishwa bungeni juzijuzi?

Wiki iliyopita nilipokuwa bungeni kwenye kazi yangu ya mchana nikakutana na hiki kitu kilichogusa sana kazi yangu ya jioni.
Kwa furaha napenda kuwatangazia wadau kuwa Bunge letu tukufu kwa mara ya kwanza limepitisha sheria ya mtoto. Nasema kwa mara ya kwanza sababu Tanzania hatujawahi kuwa na sheria ya mtoto.
Sasa wewe kama mzazi na mtanzania kwa ujumla, una wajibu wa kujua yaliyomo kwenye sheria hii, maana unaweza kujikuta unapelekwa mahakamani bila kujua na na ukaishia kulipa fine kubwa au kutupwa lupango.
Ila kwa kuwa nipo hapa kwa ajili yako, huna shida ya kuusoma msheria woooote,(si mnawajua wanasheria kwa kutumia lugha ngumu?) usijali mi ntasoma, afu ntakua nakurushia vipande kidogo kidogo kwenye blog yako pendwa kwa lugha yetu (wanatuita laymen/women) tuliyoizoea.
Hata ukitaka Mama Sitta (waziri husika) ntaenda uongea nae, kwanza tumpe hongera kwa kufanikisha hilo, maana nae ana nia watanzania wengi waijue na kuielewa sheria hii.
Kwa kuanzia, ni kwamba sheria hii ni kwa mara ya kwanza imekusanya vipengele vyote vinavyohusu mtoto kwenye sheria nyingine na kuviweka pamoja, na hivyo kutengeneza mkusanyiko wa sheria moja ya issues za watoto tu. Zamani kila kitu kuhusu mtoto kilikua kwenye sheria mbalimbali, ukitaka mirathi, basi uende sheria ya mirathi, ukitaka matunzo, sijui uende wapi, ili mradi kila kitu kwake.
Katika sheria hii, pamoja na kuainisha haki za mtoto, zinawabana ipasavyo wazazi na walezi, pia kuna wajibu wa mtoto.
Pamoja na mambo mengine mengi, pia inazungumzia kuhusu kutumikisha watoto, haki ya mirathi kwa watoto (wa nje na ndani ya ndoa) kuasili watoto (adoption) na mambo mengine kibao.
Stay tuned hapahapa, wakati nikikupa kipengele kimoja baada ya kingine.

No comments: