Tuesday, December 1

Siku ya Ukimwi Duniani: Mzazi timiza wajibu wako, namba hizi zipungue


Leo ni siku ya Ukimwi duniani, well, kila mtu anajua hilo, basi mimi nataka nikwambie vitu ambavyo inawezekana hujui, kuhusiana na Ukimwi na watoto Tanzania, takwimu hizi ni hadi kufikia mwaka 2007.
  • Watoto 140,000 walikua wanakadiriwa kuwa wanaishi na vijidudu vya Ukimwi
  • Jumla ya watoto yatima 970, 000 wazazi wao walifariki kwa Ukimwi
  • Inakadiriwa kuwa wanawake 760,000 (wenye miaka 15+) walikua wanaishi na Ukimwi, hivyo kuhatarisha maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Hiyo nguo (mi naiitaga kinyelamumo, sjui wengine mnaitaje) imeandikwa
UKIMWI: Ni tatizo la kila mmoja.
Wazazi tuepushe tatizo hili kubwa kuwa la watoto wetu kwa:
  • Kupunguza maambukizi baina yetu, ili tusiwafanya wawe yatima wa Ukimwi
  • Kupunguza maambukizi ya mama-kwa-mtoto, ili wasizaliwe wakiwa wameshaambukizwa Ukimwi
  • Kupunguza maambukizi ya Ukimwi kwa vijana, kwa kuwaelimisha watoto wetu juu ya janga hili tangu wakiwa wadogo
  • Kuwatunza na kuwalea vizuri ndugu, jamaa na marafiki wenye Ukimwi, na pia yatima wa Ukimwi
Love, Jiang.

No comments: