Monday, November 30

Utundu wa Jayson

Mdau wa siku nyingi, Jayson James, akifanya utundu.
Hapa anazima na kuwasha stabilizer, na hivyo anazima na kuwasha TV.
Watoto otee wanapenda kuzima na kuwasha vitu, hasa ambavyo wanaona effect yake hapo hapo, kama TV na taa.

Akishangilia baada ya ushindi wa kuzima na kuwasha TV. Mi nawapenda wao teletubies kwenye t-shirt.

Kahamia kwenye viatu, ni kupangua tu. Hapa ndipo mpangilio wa vitu unapokuwa mgumu ndani, maana we ukipanga yeye anapangua...

Kakamatia remote control...hapo mama sahau kuangalia vipindi vayko, hamna cha tamthilia wala nini...

Mwisho anajipumzisha kwenye chupa yake ya maziwa kama sio yeye.
Utundu unatumia nguvu nyingi, so lazima mtoto awe anakula mara kwa mara.

1 comment:

Anonymous said...

Mpaka hapa huyu nasema atakuwa Fundi Umeme tena Mkuu
hahahahaha

Hongera mama Jayson nimependa huu ni ndiyo wakati wao wa kujidai.


disminder