Sunday, December 20

Watoto wa TSN wakishangilia kombe

Yeeeeeeeeeeeeeeeeeaaah!
Xchyler akishangilia ushindi wa kampuni ya mama kwenye mchezo wa kuvuta kamba.
TSN iliwatoa na kuwabwaga chini Mwananchi.
Hii ilikua jumamosi kwenye media bonanza ya Zain.

Mdau Harieth naye alikuwepo akashika kombe kwa niaba ya mama, Regina Kumba.


Xchyler anataka kumchum Harieth, ila Harieth ashagutukia kuwa hiyo ni gia ya kunyang'anywa kombe, wala hakukubali!

Alipolishika mara ya kwanza alikua anajaribu kunywa vilivyomo, afu akakuta peupe.

X na baba na kombe la timu ya mama, ambayo baba aliipa tafu hadi ikashinda!

1 comment:

Anonymous said...

mimi nahisi X alikuwa anataka kunywa kilichomo ndani ya kombe cuz anadhani ni kama vile vikombe vya kanisani vya kunywea divai. Igogo J