Sunday, December 13

X akipunga upepo beach

Xchyler na kitu chochote kinachohusu maji humtoi, yawe ya kunywa kwenye kikombe, yawe ya kuoga au kuogelea baharini ye lazima atayachangamkia tu!
Na mimi huwa simnyimi raha, napenda kumpeleka beach mara kwa mara, hapa ni wikend flani, mwanzoni mwa mwezi huuu. Tukifika beach lazima matayarisho yote tuyafanye kwenye gari, maana yeye akiona maji ni kuyakimbilia, hata kama amevaa viatu, na mimi lazima niwe tayari tayari kwa usalama...

X alichezea sana maji na mchanga...Alikimbia huku na kule, hadi alikimbiza mbwa wa watu, uzuri ni kim-mbwa chenyewe cha kidhungu kikawa kinakimbia nae tu...picha niliikosa hapo, maana nilikua nimekaa nae, alivyoona mbwa ghafla akachomoka, na mimi ikabidi nichomoke nae.
Nnatamani mngetuona, mngecheka, maana yeye anakimbiza mbwa, afu na mimi namkimbiza yeye asije akanipotea...vichekesho!
Tulifurahi sana, ila mi niliumwa nyama za mapaja siku tatu, maana kukimbizana kwenye mchanga si mchezo...yeye mwenzangu alikua fit tu!

1 comment:

Smiles said...

Mamaaaa.....
hii nilikuwa sijaona bado....
dogo ndio maana huwa hataki kutoka kwenye shower! kumbe ndio zake....