Saturday, January 9

Happy birthday Harieth

Leo mdau Harieth Mpogolo anatimiza mwaka mmoja...jamani mdau huyu tumetoka naye mbali, tangu enzi za ma'mtu Regina Kumba kuwa model na tumbo lake kwenye dalili za mimba, mi nilidhani alishatimiza mwaka ati!
Ma'mtu kaniambia mdau anaenda kulia birthday hii kwa bibi Kigoma, mi naomba niletewe migebuka!
Sifa kubwa ya mdau ni utundu! Nahisi hata X haingii ndani hapa kwa utundu!

Mama na Mwana pamoja na wadau wooote tunamtakia Harieth maisha mema, marefu yenye kheri na fanaka tele, Mungu amjaalie sana.

1 comment:

Mama Kelvin said...

Waooh katoto kazuri jamani, mama mtu Regina hongera sana kwakukuza.