Tuesday, January 26

Mwanangu hali...

Mambo,
Mimi ni mama wenye watoto wawili huyu mkubwa karibu anafika miaka miwili lakini hataki kabisa kusikia chakula kingine zaidi ya mtori ambao umewekwa kwenye blender bila hivyo yeye siku hiyo atafunga ramadhani. Naombeni ushauri na mimi ni mama ninayefanya kazi
Mama Moses/Michelle

7 comments:

Lulu said...

Mi nadhani mama Michelle ulimchelewesha mtoto chakula, kwa kumsagia mtori kwenye blender inaweza kuwa ndo sababu hataki chakula kingine kwani akijaribu anakutana na particles ambazo zinakuwa kama zinampalia ndo maana hataki chakula chochote zaidi ya blended mtori. Nakushauri acha kublend msagie kwa mkono halafu mlishe akijitapisha unampumzisha then mnaendelea tena hadi atazoea. Ila pia kumbuka kuna watoto ambao by nature hawapendi kula. Nina mtoto (Vicent) alikuwa anakula vizuri sana kabla hajaanza kutembea, alipoanza kutembea na chakula kikawa sumu kwake, akiona chakula ni kweli anatapika kabisa hadi leo amebakia na kichwa na ngozi na mfupa lakini very active and healthy. Nakupa pole kwani najua inavyoudhi.

Anonymous said...

Pole, Mnapokula mezani Jioni, naye mtengee sahani yake mwache ajifunze kula mwenyewe, ataanza kwa kuchezea mwishowe atanyanyua kijiko kupeleka mdomoni.
Mpe hata ugali na maharage, havidhuru mamii, try this you will tel me.

mwanzoni apewe chakula kila mara coz atakuwa anakula kidogo kidogo, mwishowe atazoea.

Anonymous said...

Pole dada mwanangu alikuwa the same yaani vyakula visivyokuwa na particles anakula kama kuna particles hali.Nikangundua kuwa tatizo ni texture sasa nikaanza kumpa vyenye paticles taratibu,pia nikashauriwa niwe nampa biscuit nikawa nampa hiyo inamsaidia kuzoea texture mpya.
Watoto bwana wewe acha tu yaani akigoma kula hata wewe mama huna hamu yakula.Namshukuru MUNGU sasa mwanangu hana tatizo na texture

Anonymous said...

Nafikiri ni kipindi tu ktk process ya mtoto kukua,wangu ilibidi nimpeleke mpaka kwa Dr,akaniambia hiyo ni growth process ingawa kweli inawezekana amezoea kublendiwa chakula,lkn pia inawezekana si mpenda kula,Dr alinishauri nisije kumpa dawa za kula otherwise hataweza kula bila dawa,kwahiyo mpaka leo mwanangu kuna kipindi anakula sana kuna kipindi hataki.Asipotaka kula inabidi nimpe vitu anavyotaka ili asilale njaa huo ndio ushauri wangu kwako otherwise theres nothing much u cn do,akikataa amekataa.

Mama Kelvin said...

Namuunga mkono mdau hapo juu, unatakiwa mkae nae mezani ila Kelvin wangu anapenda mkae chini ndio anakuwa huru kula, anaanza kwakujimwagia chakula na kidogo ndio kinaingia mdomoni then anazoea nakuanza kula vizuri, watoto wanapenda kuona wanakula wengi. au kama unamtoto wa ndugu yako umri kama wake mlete uwaweke pamoja nakuwaimbia nani atamaliza kula mshindi basi wanajitahidi kula balaa ili awe mshindi.Fanya hivyo ikishindikana nitakutajia dawa fulani inasaidia kumpa hamu yakula, ingawa kumzoesha dawa mtoto pia si nzuri.

Anonymous said...

Naungana na Lulu, mama Vicent achana na kusaga chakula kwenye blender, sababu umechelewa anza sasa kumsagia na mkono, mie mwanangu nilipata ushauri kabla nilianza kumsagia na mkono zinabaki particles akiwa na miezi kati ya 5 na 6 ikawa kila anavyoendelea kukua napunguza kusaga sana mpaka sasa nimeacha kusaga anakula mwenyewe kwenye sahani yake na mapema May anatimiza miaka 2.Lingine zuri ni la kula naye mezani pamoja.

Anonymous said...

Pole mama Moses ila zingatia ushauri wa hao wenzetu waliotangulia.

Mimi nilikuwa naishi na dada yangu mwanae aligoma chakula kabisa hadi miaka miwili, tulijaribu kila njia ikashindikana basi ya mwisho ikabidi huyu dada nilokuwa naishinae amuombe mtoto wa dada yetu mkubwa ambaye umri wao ulikuwa sawa.


Dada mkubwa kwakumuonea huruma mdogo wake ilibidi ampe mtoto wa miaka miwili akamchangamshe mwenzie kwani alikuwa nae amebaki kichwa na macho tu. Basi hapo ilikuwa ni mashindano kwani mgeni alikuwa mlaji basi kwakugombea ushindi mbona kila mtoto alikuwa mshindi hadi mboga za majani.

Na baada ya mlo walipata icecream lakini sio mara kwa mara. Ilimsaidia sana asiyependa kula na dada yangu aliondoa stress kwani ni mfanyakazi kwama wewe.

Jaribu nawe umuokoe mtoto. Sina mtoto lakini napenda sana kuitembelea hii blog sababu nawapenda akina mama na watoto.

Naomba mungu nipate wangu ili niendeleze libeneke live na nyie.