Thursday, February 11

Majina kumi yanayoongoza kwa wamarekani-waswahili

Haya ni majina kumi yaliyotumika sana kwa wamarekani -waswahili (African-Americans/blacs) kuwapa watoto wao huko US.
Majina ya Prezida na Fist Lady wao nayo yamo.

(yenye rangi tofauti kuna mdau mwenye jina hilo)

Ya Kike:


1 Madison
2 Kayla
3 Makayla
4 Michelle
5 Nevaeh ( hili ni heaven limegeuzwa, naipenda hii style)
6 Jada
7 Brianna
8 Chloe/Khloe
9 Alyssa/Destiny (yamegongana)
10 Gabrielle/Imani (yamegongana)

Ya Kiume
1 Jayden 2 Joshua 3 Elijah 4 Jaden 5 Justin/Christian (yamegongana)
6 Jeremiah
7 Isaiah 8 Jordan 9 Christopher/Michael (yamegongana) 10 Barack (Kibongo ni Baraka)

*****
Ningependa sana niweke majina kumi yaliyoongoza Tanzania na sisi tujue jina gani liko juu kwetu, ila siwezi kuweka vitu toka hewani, hawa wenzetu wanatoa kwenye statistics zao maana mtoto anapozaliwa tu, anaandikishwa.
Mimi nna uhakika watoto wengi tu hawajaandikishwa RITA, acha waliozaliwa mwaka jana, labda hata ma mwaka juzi bado, hasa hasa kuna namba tu ya watoto waliozaliwa, kwa hiyo siwezi kujua majina gani yaliyoongoza kwa kupewa watoto mwaka jana nchini kwetu.
Hadi ukiritimba na kutumia makaratasi badala ya komputa kwenye idara za serikali uishe ndio vitu hivi vutakua rahisi kuvifanya.
NB: RITA mna ushirikiano na mnajitahidi sana kuboresha mambo, hasa CEO, Mr Saliboko, ila system nzima inachosha sana, maana kila kitu ni karatasi, unatafuta hadi unasikia kizunguzungu!

No comments: