Monday, February 1

Mtoto akitoka meno ni lazima aharishe?

Hello Jiang,
hivi mtoto akitoka meno ni lazima aharishe?
Jamani Imar wangu anaharisha mpaka amepungua, anatia huruma hali vizuri mpaka ninakosa raha mwenzenu, nimempeleka kwa daktari amepewa dawa basi kupeana hizo dawa ni issue hataki hata kuzisikia,vijino 2 vimeanza
kujitokeza lakini huko kuharisha balaa.
Regards, Mariam.

*****
wadau naomba mchangie,
sio nia yangu kutotoa mchango, ila huku Dodoma nabanwa sana, pia naamini wadau mnatoa michango yenye kuelimisha sana, kama ile ya mtoto kutotaka kula, na hivyo mnaweza kumsaidia Mariam na wengine wenye tatizo kama hilo, mi ntaingiza neno nikiona hamna suluhisho linalofaa sana, ila hadi sasa experience zenu zinasaidia sana kutoa suluhisho.

8 comments:

Lulu said...

Mama Imar, pole sana kwa kuuguliwa na mtoto, mpe pole mtoto na inshallah Mungu atamsaidia atapona. Kuhusu kuwa mtoto akianza kuota meno ni lazima aharishe si kweli kabisa, ila kuota meno na kuharisha vyaendana kwasababu mtoto anapoanza kuota meno huwa anawashwa zile fizi zake sasa njia pekee pekee ya kujipa relief na huo muwasho ni kuweka vidole na vitu vingine mdomoni, sasa hapo ndo kuhara kunapokuja kwani ataweka vidole vichafu mdomoni na vitu vingine vichafu pia vitapita mdomoni. Ki ukweli kunywa dawa itakuwa ngmu kwani kwanza atakuwa na maumivu kwenye fizi lakini pia kama ni mvivu kula by nature basi ndo atazidisha kwa sababu ya kale kahoma na kuharisha. Ni hayo tu ndo ninayoyajua.

Anonymous said...

pole sana,mariam kwa mtoto kuumwa.Ukweli ni kwamba sio lazima mtoto akiota meno awe ana harisha au apate homa.Tatizo hilo linajitokeza hivyo kwakua kipindi mtoto anaota meno fizi zake huwa zinawasha hivyo mtoto anakuwa anaokoto chochote na kuweka mdomoni ili kijikinia fizi,na unakuta kitu hicho sio safi ndipo mtoto anapata bacteria ambao wanamletea hayo matatizo.Mtu asikundanganye kuwa ni kawaida mtoto kuarisha pindi anapo ota meno.Jitaidi kuangalia mazingira anayo penda kutambaa na kuyaweka safi.Muone Dr.atakupatia dawa na hata akikupatia dawa,KUMBUKA KINGA NI MUHIMU KULIKO DAWA,WEKA MAZINGIRA SAFI KWA MTOTO WAKO.

Aunt Maggie

mama bethania said...

kuna dawa inaitwa Ashton powder hiyo ni ya unga unampaka kwenye fidhi kabla meno hayajotoka mpaka yanapotoka hata harisha wala kuchemka kwa homa na hamu ya kila haipotei.

Anonymous said...

HI
MI NAONA INATOKANA NA MTOTO MAANA MIE WATOTO WANGU HAWAJAWAHI KUHARISHA MAANA NIKIONA TU WANADALILI ZA KUPATA MENO HUWA NANUNUA DAWA IKOM KAMA POWEDER NA MSUGULIA MTOTO HAPATI HOMA WALA KUHARA SASA SIJUI HIYOU DAWA NDIO INASIDIA AU NI MTOTO MWENYEWE

POLE SANA MUNGU ATAMSAIDIA ATAPONA ISHALLAH

Anonymous said...

Sio lazima mtoto akiota meno lazima aharishe....anaharisha kwasababu anaokota vitu chini na anavitumia kukunia meno,inatakiwa uwe mwanagalifu na mazingira yawe masafi ...pia mtoto akiharisha hakikisha unampa maji ya kutosha asiwe dehydrated....kama dawa hapendi chemsha mchele yale maji ya wali (rice water) mpe...usiweke chumvi ataacha kuharisha

Anonymous said...

INATEGEMEA NA WATOTO,wengine wanaharisha na wengine wanadunda tu.Mwanangu hakuharisha vile viwili vya chini,ila sasa mengine yanatokea mawili chini na mawili juu kwa kweli aliharisha siku moja tu ila homa ilimpata sana homa ilikuwa ni 39°C hadi 40°C kama siku tano hivi nilimpeleka hospitali sana sana tulipewa paracetamol tu na tukawa tunamsponge.
Hapa kwa kweli inategemea na mtoto ila wengi wanaharisha na kupatwa homa.
Mama Jéjé

Mama Kelvin said...

Pole sana naweza kusema havihusiani mtoto kuharisha sababu yakuota meno, sema mtoto anakuwa anaokota vitu vya kuweka mdomoni ili asugue fizi zake vinakuwa vichafu, kama utaweka mnunulie nyonyo bandia aweke mdomoni ila liwe safi atakuwa anangatangata ndio anajikuna kiaina, na kuhusu homa mpe cafenol ya kidogo ya watoto ni nzuri sana kwa homa.

Anonymous said...

Pole sana mama, naomba nichangie solution ya kupooza kwa muasho wa fizi za mtoto anayeota meno. Safisha vizuri chupa ndogo ya maji, halafu iweke kwenye friji, maji yakipoa chupa pia itakua imepoa, ukimuona anahangaika kutafuta kitu cha kutafuna mpe hiyo chupa mtoto aichezee (aitafune tafune hiyo chupa ndio maana ioshwe vizuri). Ule ubaridi wa chupa unapooza kuwashwa. Jaribu.