Tuesday, March 23

Usafiri hatari...tunaweza kuubadilisha!

TotoCam ilimnasa mdau akiwa amepakiwa kwenye baisikeli hivi karibuni.
Tatizo ni jinsi alivyojishikilia...hamna usalama kabisa hapo!!!
Hii ndio njia sahii ya kumbeba mtoto kwenye baisikeli, kwanza anakua mbele so anaona kila kitu (maana kama X asivyopenda kupetwa ukimuweka nyuma lazima akusumbue) na pia anakua kwenye upeo wa macho yako, unaweza kuona chochote kinachomtokea kuliko akiwa nyuma hata nguo yake ikinasa kwenye mti hujui! Naamini viti hivi vikiwepo wazazi hawataona tabu kuvinunua na kuwawekea watoto wao kwa usalama zaidi.

2 comments:

Anonymous said...

Inapendeza sana. lakini wiki iliyopita kuna baba alikuwa amepakia mwanaye kwa nyuma kama hiyo picha ya mwanzo.

Sasa njia tuliyokuwa tunapita ina magari makubwa ya michanga na daladala nyingi. Kusema kweli hiyo njia ni fujo tu.
Yule mtoto kapanda lakini macho yake yote yako nyuma kuangalia magari yanayowafuata na unamhisi ana uoga kabisa.
Gari yetu ilipokuwa inawakaribia ili tuwapite, mtoto akataka kuachia na kuruka. Ikabidi tumwambie baba yake awe makini sana kwani yale magari ya michanga na daladala ndiyo fujo kabisa.
Na mtoto tukamwambia asiangalie nyuma.

Ndiyo usafiri wetu lakini ni hatari sana kwa watoto kukaa hapo nyuma.


disminder.

tayana said...

pia kanaweza kusinzia jaman kakajiachia..loh hatari sana