Showing posts with label Tafakari. Show all posts
Showing posts with label Tafakari. Show all posts

Tuesday, March 23

Usafiri hatari...tunaweza kuubadilisha!

TotoCam ilimnasa mdau akiwa amepakiwa kwenye baisikeli hivi karibuni.
Tatizo ni jinsi alivyojishikilia...hamna usalama kabisa hapo!!!
Hii ndio njia sahii ya kumbeba mtoto kwenye baisikeli, kwanza anakua mbele so anaona kila kitu (maana kama X asivyopenda kupetwa ukimuweka nyuma lazima akusumbue) na pia anakua kwenye upeo wa macho yako, unaweza kuona chochote kinachomtokea kuliko akiwa nyuma hata nguo yake ikinasa kwenye mti hujui! Naamini viti hivi vikiwepo wazazi hawataona tabu kuvinunua na kuwawekea watoto wao kwa usalama zaidi.

Monday, March 22

Tafakari: Omba omba watoto

Kama ombaomba wakubwa walivyoenea kwenye kila kona ya kila mji mkubwa, siku hizi kuna mfumuko mkubwa wa ombaomba watoto.
Wanaowapa wanawapa shingi 100, 200, 500, au chochote mtu alichonacho, na watoto hawa hushinda kwenye jua siku nzima wakifanya kazi hii ya kuomba.
Saa nyingine wazazi wako pembeni wakionekana kabisa, saa nyingine wazazi wako nyumbani, watoto wanahangaika mijini.
Afu kuna wale wanpenda sana kukaa Morocco jioni hadi usiku, saa nyingine hadi saa nne usiku, wadada wamebeba vichanga, huku wanaomba.
Ila hata ukipita ukampa noti ya alfu kumi kila siku asubuhi na jioni, hilo sio suluhisho la tatizo hili, maana swali ni kwamba wakiwa wakubwa watafanya nini? maana wakati wenzao wakiwa shule wanasoma kuwa kitu chochote wakiwa wakubwa, hawa wanaomba barabarani siku nzima, learning nothing.
Najua sio kosa lao, maana sidhani kama ukimpeleka shule atakataa, kosa ni la wazazi, wala hao wazazi wasisingizie umaskini, I know for a fact kwamba wanapata zaidi ya anachopata mlinzi mwisho wa mwezi! 
Ila kama wazazi hawawapi watoto haki zao za msingi, kitengo cha huduma za jamii wanafanya nini kuwanusuru?
Na hii si ajira hatarishi kwa watoto, wanaoshughulikia haki za watoto hawawaoni hawa?