Friday, April 30

Collins kasimamia harusi...

Hili pozi kali ndani ya suti si la bure, mdau Collins Johnson alisimamia harusi ya Uncle wake hivi karibuni!
Sasa soma story mzima ya ilivyokua kama anavyohadithia ma'mtu, Judith Rwakyendera baada ya hiyo picha...


Nimeona nishee picha za Collins Johnson alizosimamia harusi ya uncle wake,tarehe 4/4/2010...
maana nayo ilikuwa experience mpya kwake, na kwetu pia kama wazazi pamoja na familia yaetu maana ilikuwa ni couching kuanzia kwa bibi, aunties na uncles wake, jinsi ya kutembea, smile,kubehave na vitu vya namna hiyo.


Kiukweli nilikuwa na hofu maana huyu kijana hawezagi kutulia sehemu moja, kutembea kwake ni nusu ya kukimbia..afu sikuwahi kumweka mbele a watu wazima so sikujua confidence yake mbele za watu.. mama X nilikuwa na hofu honestly.


Alinipa mshangao alivyotulia,kuanzia kanisani mpaka ukumbini,ingawa alifanyafanya makeke kidogo(eti akitaka kukojoa anatoka moja kwa moja mpaka kwa baba! huwa hapendi jinsia ya kike imuone akiwa mtupu(naruhusiwa mimi tu na bibi basi)
 Ila alilalamika kwa nini yeye na bi harusi mdogo wamenyimwa ule mkate wa kanisani...ilibidi babaake aanze kutoa maelezo tena.


Alipopewa nafasi ya kulishana keki(kwa bahati mbaya picha sikupata) sijui nani alimfundisha staili ya kushika bega..akakamata bega la bi harusi mdogo akamlisha kitu ambacho kilifanya ukumbi mzima uangue kicheko.
 
 (Anamchum mom)
It was fun,the suit,the couching,the event ilifanya familia nzima ichangamke.Am very proud of him
and guess what.. watu watatu wanataka akasimamie tena kwenye harusi zao..ingawa sitakuwa na nafasi.labda kwa couple moja tu afu basi.

***

4 comments:

Anonymous said...

kwakweli nimecheka saana baada ya kusoma ishu ya kulishana keki....labda kaona sehemu
mama D

Natujwa said...

Jamani huyu mdau ni handsome...alipendeza sana. Ma mtu Judith Rwakyendela wa Zanaki? jamani amekuwa mdada, kweli umekuwa shost mpaka una mtoo mkubwa namna hii.congrats

mama Collins said...

Mama D mpenzi,
I guess your right, maana Collins ni visual learner...ila sijawahi kwenda naye kwenye harusi au labda kwenye mikanda ya harusi ya familia.

Yani kusema ukweli wakati mwingine huwa siamini kama mwanangu amekuwa kiasi cha kufanya vijimaamuzi fulani hivi bila kufundishwa..ila namshukuru mungu maana ni baraka za pekee ukiwa unaona malaika wako akichukua step mpya kila kukicha,inakufanya uwe unachungulia tumbo lako kila siku ukijiuliza "eti juzi tu alikuwa tumboni mwangu" akina mama wenzangu ulishawahi kuwa na hiyo feelings?

Anonymous said...

Hongera zake mtoto kwa kusimamia arusi. Mimi sio shabiki sana wa kuwafanyia mafunzo ya pekee watoto wanaosimamia arusi na siku nyingine jaribuni kuwaacha watoto wawe huru mtaona inavyopendeza. Mimi mwanangu alisimamia arusi siku mbili tu baada ya birthday yake ya miaka mitatu. Wato wote waliomuona kabla walikuwa wanabisha kwamba hawezi kusimamia arusi, lakini yeye mwenyewe alikuwa anasema "nasimamia arusi, nakaa na bwana arusi" basi hatukumfanyia mafunzo yeyote na alifanya kile anachofanya mtoto yeyote, ilipendeza sana, yaani pale mbele ilikuwa mara ashuke chini kuokota visoda na kuanza kuchezea, mara aende huku, ili mradi anacheza akamwambukiza na yule msichana nae. Ilipendeza sana kwa watu walioona ile arusi.