Tuesday, April 6

Khloe azaliwa upya katika Yesu

Mdau Khloe Mfumu amezaliwa upya kwa kubatizwa Jumapili ya Pasaka, katika kanisa Katoliki la Segerea, kigango cha Kinyerezi...hicho kigauni kiko cuuuute!

Maji na kibaridi hiki, alishtuka huyo...

...bado haamini kama ameogeshwa na nguo zake...dady kafurahi...

...na mumy nae kafurahi...

...akiwa na ma'mtu, Rosemary na ba'mtu Innocent...

hii hatua huwa naipenda sana, wadau huwa wanaushangaa mshumaa mno...

wakati wa kupakwa mafuta na Padre...

Mdau akiwa na baba na mama baada ya shughuli kuisha, sasa kazaliwa upya katika kanisa.

Bib'mtu Hilda Maliti naye alikuwepo kumsindikiza mdau...bibi na mjukuu tena, hasa akiwa mjukuu pekee toka kwa mtoto pekee, kama mboni ya jicho vile!

mdau akiwa na mama wa ubatizo aka Godmother, Auntie Bertha.

*****
Mama na Mwana inamtakia mdau Khloe maisha mema ya kiroho na aongozwe na Yesu siku zote.

1 comment:

I-Love-kids said...

Bwana Yesu akufunuke kwa baraka zake,ukue kimo na akili.Roho yako iwe nyeupe kama theluji siku zote za maisha yako.Uishi na kudumu katika Kristo hadi siku utakayorudi mavumbini.