Friday, April 30

Matokeo Form Six: Ni Marian Girls tena

Shule ya Marian Girls inaendelea kuongoza kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ambapo imeongoza kwenya matokeo ya kidato cha sita mwaka huu yaliyoangazwa  leo mchana.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako amezitaja shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 30  na zaidi kuwa ni:
   1. Marian Girls (Pwani)  
   2. Mzumbe (Morogoro)  
   3. Uru Seminari (Kilimanjaro)
   4. Kibaha (Pwani)
   5. Feza Boys (Dar es Salaam)
   6. Tabora Boys (Tabora)  
   7. Tukuyu (Mbeya)
   8. Kifungilo (Tanga)
   9. Ilboru (Arusha)  
  10. Malangali (Iringa)

 Kwa upande wa shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 30 ni:
   1. Rubya Seminary (Kagera)
   2. Maua Seminary (Kilimanjaro)
   3. St. James Seminary (Kilimanjaro)
   4. St. Joseph Kilocha (Iringa)
5. Dungunyi Seminary (Singida)
   6. Same Seminary (Kiliomanjaro)
   7. Usongwe (Mbeya)
   8. St. Peter’s Seminary (Morogoro)
   9. Viruka (Dar es Salaam)
   10. Vwawa (Mbeya)

Ndalichako alizitaja shule kumi zilizoshikilia mkia katika kundi la shule zenye watahiniwa 30  na zaidi  kuwa ni High-View International (Unguja) Fidel Castro (Pemba), Sunni Madressa (Unguja), Neema Trust (Dar es Salaam) Mtwara Technical (Mtwara), Mureza (Tanga), Tarakea (Kilimanjaro) Uweleni (Pemba), Arusha Mordern (Arusha) ya kumi kutoka mwisho ni Maswa Girls (Shinyanga).

Katika kundi la shule zenye wanafunzi pungufu ya 30, ya mwisho kabisa ni Nkasi (Rukwa), Maont Kilimanjaro (Kilimanjaro), Mbarali Preparatory (Ungunja), Lilian Kibo (Dar es Salaam), Ghomme (Dar es Salaam), Adolec (Kagera), Mzizima, Dar es Salaam Christian Seminary na EDP Royal za Dar es Salaam na Sekei ya Arusha.

No comments: