Wednesday, May 19

Glory's birthday party, ilikua red!

 Malaika huyu si mwingine bali mdau Glory, siku ya birthday party yake, kusherehekea kutimiza miaka miwili Jumamosi iliyopita...msimtamani sana, X keshaanza kuwekeza hapa!

...ingawa hapa amenuna, lakini amependeza!

pozi la full, naona ilikua mambo ya red & white, sikujua kama hayo mabawa yako rangi mbalimbali, naonaga white na baby pink tu!
Glory na Jackline...hawa nao muda si mrefu watakua mtu na dada'ke!

Glory anamlisha mama tamtam...Jack umenibania picha ya tamtam!

...sherehe za wadau bila mambo ya kulia ujue haijaisha!

sherehe ilifanyikia nyumbani kwa bibi na babu yake pale ubungo river side, hata ya mwaka mmoja ilikua hukohuko, mabibi walivyo bize na wajukuu, hadi raha!

wametoka bomba, mtu na mama'ke! Tatizo ni mdau kanuna, akicheka anavyokuaga mzuri sasa!

No comments: