Wednesday, May 19

Karen, salamu toka kwa mama

Mdau mpya, anaitwa Karen, huu ni ujumbe toka kwa mama yeka, Grace Gabriel.

Mimi naitwa Grace, mwanangu anaitwa Karen. Nasoma na kufanya kazi na naishi hostel ili kuweza kumudu shule na kazi kwa urahisi. Nilianza kuwa bize na shule siku tano tu baada ya kujifungua ili kuweza kufanya mitihani na nilihama kabisa nyumbani kurudi kuishi hostel miezi mitatu baadaye.Namshukuru sana mama yangu kwa kunilelea tangu day one hadi leo.Mtoto wangu amekua na tena ana furaha na afya nzuri.

Napenda ajue daima kuwa umbali unaokuwa kati yetu kwa vipindi fulani vya maisha kamwe hauwezi kubadili wala kupunguza mapenzi niliyonayo juu yake.Naguswa sana na blog yako,ni lazima nipite humu kila siku,smile za watoto nizionazo humu,ukuaji wao na ukaribu wa mama na watoto wao,hv vitu vinanipa matumaini na furaha ya ajabu na kuniunganisha sana na mwanangu kimawazo.

*****

Grace kazana umalize shule, maana ndio unamtengenezea maisha mazuri ya baadae Karen, na wala hatokulaumu kwa hilo, maana unalofanya ni jambo la muhimu sana, na daima atakushukuru kwa hilo. Hongera sana kwa kusoma na kulea, hata kama ni kulea kimawazo tu, pia hongera kwa bibi kwa msaada mkubwa anaokupa, Mama zetu waache tu waitwe mama, wanayotufanyia ni makubwa sana, na hatuna cha kuwalipa zaidi ya kusema Asante mama.
Jiang.

1 comment:

Grace said...

Thanx Jiang.Salamu kwa X na ubarikiwe sana